Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 19 December 2014

DR MANDAI AKIWA NA MKUU WA WILAYA ILALA KATIKA HAFLA YA KUTOA MADAWATI

        Dr Mandai kushoto akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Raymond Mushi

Mandai Herbal Clinic katika shughuli zake za kutibu watanzania kwa kutumia Tiba Asilia pia haijasahau majukumu yake katika kuhakikisha kuwa jamii iliyopo inaishi kwa kupata elimu iliyo bora na yenye kukidhi viwango hivyo ikaona ni vyema kutoa msaada wa Madawati 60 yenye uwezo wa kukaliwa na wanafunzi 240 katika shule ya msingi Mongo la ndege iliyopo Ukonga Mombasa 
            Madawati hayo yalikabidhiwa kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mr Omary  na kutoa shukrani zake za dhati kwa niaba ya wanafunzi na wazazi wa bodi ya shule kwa Dr Mandai kwa kusema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa watanzania wengine kwani si kila kitu lazima tuisubiri serikali ije kufanya na kuwaomba wakazi wengine wa ukonga kuiga mfano huo ili kuhakikisha jamii yetu inalelewa katika misingi iliyo bora ya elimu na mshikamano ulio thabiti.

No comments:

Post a Comment