Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 23 January 2015

DAWA ZA ASILI ZINATHAMANI SANA NI VYEMA ZIKAHESHIMIKA Dk Mandai akiwa porini katika harakati za kutafuta dawa kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania kupitia kituo chake cha Mandai Herbalist Clinic.
Tunapozungumzia dawa asili moja kwa moja tunakuwa tunagusa suala la tiba asili zilizotumika enzi za mababu. Kipindi hicho tiba za kisayansi kwa maana zile za hospitali ambazo zinapatikana kwa sasa katika maeneo mengi hapa nchini na duniani kote hazikuwepo.Kipindi hicho cha kale wale waliokuwa wakisumbuliwa na maradhi mbalimbali walikuwa wakitegemea tiba za asili, ambazo zilikuwa zikitokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo ni pamoja na miti ya asili iliyokuwa ikipatikana kwa wingi kutokana na kutokuwepo kwa uharibifu mkubwa wa misitu kwa wakati huo kama ilivyo kwa sasa.

Ni wazi kwamba kumekuwepo na mimea maarufu katika jamii zetu ambayo tumekuwa tukiitumia kama dawa, miongoni mwa mimea hiyo ni pamoja na mwarobaini na mlonge. Ingawaje miti hii imekuja kuwa maarufu zaidi miaka ya hivi karibuni baada ya tafiti mbalimbali kubainisha kuwa dawa za kizungu licha ya kusaidia kutibu, lakini pia zinaweza kuacha athari mbaya kwa mtumiaji.

Kumbukumbu zilizopo ni kwamba, mara baada ya kuingia kwa tiba za kisayansi mkazo mkubwa ulielekezwa katika matumizi ya dawa hizo na kujikuta jamii ikizipa kisogo kabisa dawa za asili kwa madai kuwa hazikuwa zimefanyiwa utafiti.

Mmea aina ya mlangmia au mtotokanga au jina jingine mtondokezi hii ni miongoni mwa mimea ambayo ilitumika sana enzi hizo katika kutibu magonjwa mbalimbali.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema, mmea huo ni wa ajabu sana na ni miongoni mwa mmea ambao hauna shina, huku akibainisha kuwa chanzo cha mmea huo ni kiazi ambapo baada ya kamba huchomoza na kutoka ardhini na kisha kujizinga katika mti na baadaye kiazi na kamba hiyo huachana.

“Mlangamia au mtotokanga ni mti wenye maajabu sana na hauna shina, lakini unasambaa juu ya mti, huku ukiwa umestawi vizuri,” alisema Dk  Mandai.

Aidha, Dk Mandai anaendelea kueleza kwamba si rahisi kiazi cha mmea huo kuchimbwa na mtu wa kawaida labda awe ni mzee au mwenye utaalam kuhusu mambo ya tiba asili.

Anasema mmea  huo unasifika kwa kutibu magonjwa ambayo watu wanasumbuka nayo, lakini wakienda hospitalini kupimwa hayaonekani.

Dk Mandai,  inafafanua kuwa kiazi hicho kinatibu magonjwa ya moyo na hasa moyo uliopanuka, huku akiongeza kusema “kwamba wazeee wetu walitumia sana mmea huu kuondokana na magonjwa ya moyo,” pia anasema wengine walitumia mmea huu kwa watoto wazito wa kutembea, ambapo walikuwa wakiwafunga kamba za mti huu kiunoni na walikuwa wepesi wa kutembea.

“Kwa wale wenye matatizo ya kukohoa kikohozi kikavu kabisa hadi wakati mwingine wanatoa machozi dawa hii huweza kutibu kabisa hadi mtu anapona kabisa,” anaeleza. 

Pia Dk Mandai anaendelea kueleza kuwa dawa hiyo husaidia kwa mtu mwenye tatizo la kukaukiwa sauti, anayesumbuliwa na athma, ambapo anasema ile kamba ikichemshwa na mtu wa tatizo hilo akitumia maji yake anapona.

Mbali na hayo, Dk Mandai anaeleza kuwa mmea huo ni suluhisho la matatizo ya kinamama pia hususani kwa wale wenye matatizo ya kukosa nguvu wakati wa kujifungua, ambapo anaeleza kuwa mama mwenye matatizo hayo anapochemshiwa kamba za mmea huo kisha akanywa maji yake basi mama huyo atajifunguwa kwa urahisi bila shaka.

Hali kadhalika anaongeza kwamba, kwa mama mwenye changamoto ya kutokuwa na maziwa ya kutosha kumnyonyesha mtoto wake, mmea huo pia ni msaada mkubwa iwapo mama huyo atakunywa maji ya dawa hiyo baada ya kuchemshwa.

Aidha, unaponya magonjwa mengine sugu kama kusafisha figo na mapafu, ambapo anasisitiza kuwa unatibu magonjwa hayo kutoakana na maajabu ulio nayo.
Dk Mandai hapa akionesha namna mmea huo wa mlangamia ulivyo


Dk Mandai anasema kwamba, watu ni vizuri wakaziamini tiba asili , lakini anasisitiza kuwa tiba asili si uchawi bali ni tiba kama zilivyo nyingine  na kuongeza kwamba mara zote dawa hizo huwa hazina madhara kama ilivyo kwa dawa za kisasa.

Sambamba na hayo, Dk Mandai anabainisha kwamba Afrika Kusini palipo na hospitali moja au zahanati ya serikali pembeni kunakuwa na kituo cha tiba mbadala ambapo hospitalini wanaposhindwa wanamruhusu mgonjwa kutumia tiba hizo kwa sababu wanaamini kuwa tiba asili nazo zinamchango wake.

Kwa kuhitimisha Dk Mandai kupitia kituo chake cha Mandai Herbalist Clinic anatoa wito kwa wale ambao wanateseka na maradhi mbalimbali  na kuwataka kutokata tamaa na badala yake wafike kituoni Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam watamuona na wanaweza kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment