Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 22 January 2015

DK MANDAI ANAKUJUZA KUHUSU UGONJWA WA KIHARUSI
Unaposema mtu fulani ana ugonjwa wa kiharusi maana yake kitaalam ni pale endapo viungo vinakuwa vimepata ganzi (stroke) na hivyo kusababisha mwili  kushindwa kujiweza na mara nyingine huweza kusababisha mtu kupata ulemavu katika kile kiungo ambacho kitakuwa kimekubwa na ugonjwa huo.


Hata hivyo, ugonjwa huu dalili zake huweza kujitokeza ghafla na mara nyingi hutoweka ghafla pia. 

Kinachosababisha kiharusi
Bila shaka wengi wangependa kufahamu ni sababu gani inayopelekea mtu kuweza kupatwa na kiharusi , Dk Abdallah Mandai kutoka kliniki ya Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam, anasema kinachoweza kusababisha ugonjwa huu ni pale ambapo eneo la ubongo linapokosa damu ndani ya saa 24 au zaidi, jambo ambalo linasababisha wazungu kuuita ugonjwa huu ‘brain attack’ au ‘stroke.’

Aidha, Dk Mandai anaendelea kusema mtu huweza kupatwa na kiharusi endapo ikatokea kuna kizuizi katika mwili ambacho kitaweza kusababisha damu isiweze kusafiri katika mishipa na hivyo kusababisha kupasuka kwa baadhi ya nyama muhimu kwenye ubongo ambazo kitaalam huitwa ‘vital brain tissue.’

Anaeleza kuwa hali hiyo inapojitokeza huwa haina tofauti sana na inapotokea mishipa ya ‘arteri’ inapopasuka na mtu huyo hukubwa ghafla na ugonjwa wa moyo, ambao kitaalam huitwa ‘heart attack’

Aina za kiharusi
Aina ya kiharusi hutokea kutokana na mshipa uitwao ‘artier’ unapoganda damu. Hali hii inapotokea damu hushindwa kusafiri kwenye ubongo, hivyo mtu kukubwa na kiharusi kiitwacho ‘ischemia neon’ hii humaanisha kuzuia damu kwa lugha ya kigiriki.

Dk Mandai anaeleza kuwa hali hiyo inaweza kutokea kwa kusababishwa na kitu kinachoitwa ‘thrombosis’ ambapo damu huganda kwenye mshipa mkubwa wa ‘artier’ mshipa huu ni muhimu sana katika mwili wa binadamu kwa kuwa ndio unaosafirisha damu kupeleka katika ubongo.

 Pamoja na hayo, Dk Mandai anasema, hali hiyo huweza kusababisha vimirija vidogo vidogo vinavyopeleka damu katika ubongo kuziba ambapo kitaalam hali hiyo nayo huitwa ‘lacunars stroke.’

Hata hivyo, aina hii ya kiharusi ‘lacunars stroke’ wataalam wamegundua kuwa haina madhara makubwa sana kwa mtu ambaye amekubwa nayo.

Kiharusi cha ‘hemorrhage’  mtu huweza kukubwa na aina hii ya kiharusi mara baada ya kupasuka kwa mishipa kwenye ubongo na kusababisha damu kuvuja yaani ‘hemorrhage.’

Hali hii inapojitokeza ni kwamba damu iliyovuja hukandamiza ubongo hali ambayo husababisha uharibifu mkubwa kwenye ubongo, kwani ubongo mi kiungo laini sana katika mwili. Hivyo kitendo cha damu hiyo kuganda katika ubongo, mbali na kuharibu eneo hilo katika fuvu lakichwa pia husababisha uharibifu wa chembe hai kwenye ubongo na hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa, ambapo hali hiyo huitwa ‘cerebral’/ ‘hemorrhage’ ambapo uvujaji wa damu hufanyika ndani ya ubongo.

Mbali na hayo, dokta anabainisha kuwa pia mtu huweza kukutwa na tatizo hili baada ya kupasuka kwa mishipa ya damu, ambao unazunguka ubongo, huku hali hiyo inapotokea kitaalam ikiitwa ‘sabarachindid.’

Ushauri na tiba
Mgonjwa mwenye kiharusi anapaswa awahishwe hospitali na ni vizuri kuhakikisha kichwa chake kinainuliwa kidogo ili kumsaidia mate yasiweze kumpalia mgonjwa.

No comments:

Post a Comment