Tuesday, 20 January 2015

EMBE NI KIBOKO YA MAGONJWA
Makabila mengi hapa nchini miembe kwa ajili ya matunda, matunda ya miembe yanayojulikana kama embe ni maarufu sana hapa nchini.

Embe ni tunda lenye ladha nzuri nap engine inweza kuwa ni moja ya sababu ya tunda hilo kulipatia umaarufu kataka jamii na hivyo watu wengi kulistawisha zao hilo zaidi.

Kuna aina nyingi za embe zinazostawishwa hapa nchini miongoni mwa hizo ni pamoja na embe dodo, embe maji, embe bolibo, embe nuka na embe sikio la punda.

Embe huliwa kama lilivyo lakini pia huweza kutengenezwa na kuwa juisi ambayo mara nyingi inakuwa na virutubisho vinavyopatikana kutoka katika tunda hilo.

Lakini Dk Mandai anasema kwamba mmea huo una faida nyingi kuanzia mizizi, shina, majani na hata maua yake.

Anasema kwamba majani ya mwembe yanatibu maradhi ya pumu na harufu mbaya ya mdomoni na yanapotumika ipasavyo huwa na uwezo wa kutibu malaria sugu.

Chukua majani ya mwembe na uyakaushe katika kivuli ili kuepuka kuondoa alkolaidi iliyomo ndani ya majani hayo ambayo ni muhimu sana katika tiba .

Dk Mandai na anasema “unaweza kuwa mtu mtanashati kwa namna ya yoyote ile lakini kama unatatizo la kutoa harufu katika kinywa bado thamani yako itapungua , hivyo tumia majani ya mwembe amabayo ni suluhisho la tatizo lako”

Aidha, Dk Mandai anaongeza kuwa wanawake wengi ambao wananyonyesha hukabiliwa na tatizo la kuwa na uhaba wa maziwa,  hivyo maua ya mwembe ni moja ya njia nzuri ya kukabiliana na tatizo hilo.

“Unga unaotokana na maua ya mwembe ukichanganywa na maji ya moto  au asali ama maziwa unasaidia kuondoa tatizo hilo,” alisema Dk Mandai

Mbali na hayo akizungumzia tunda lenyewe anasema linasaidia sana katika usanisi wa chakula tumboni kwa kuwa limesheheni  vitamin A,C,D.

“Katika embe kuna kiwango kikubwa cha madini ya chuma na chumvi, tunda hili pia linaongeza hamu ya kula chakula kwa anayelitumia"

Hali kadhalika Dk Mandai, anasema kwamba kokwa la embe lenyewe pia husaidia sana kwa akina mama katika tatizo la uzazi.

Dk Mandai anasema kokwa “Linazibua mirija ya uzazi na linabalansi hedhi ya mwanamke hususani kwa yule ambaye anakwenda bila mpangilio” aidha, “aliongeza kuwa twanga kokwa, unga wake tumia katika maji moto inazibua mirija ya uzazi  na inazuia utokaji wa damu na kuondoa uvimbe katika tumbo la uzazi “  alisema.

Kwa uchache hizo ni faida za mwembe, hivyo ni vizuri tukajenga tabia ya kupenda dawa zetu za asili kwani bado zina tija katika kuhakikisha zinarekebisha afya zetu, lakini kumbuka kwamba endapo unasumbuliwa na maradhi yoyote ni vizuri ukafanya maamuzi sahihi sasa ya kufika Mandai Herbalist Clinic na kukutana na Dk Mandai na uweze kupata suluhisho la tatizo lako la kiafya kupitia tiba halisi za mimea asilia.

No comments:

Post a Comment