Thursday, 29 January 2015

FAHAMU JUU YA UGONJWA WA KISUKARI NA VYANZO VYAKEUgonjwa wa kisukari ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza, lakini ni tishio kwa watu wengi kwa sasa. Ni tishio kwa sababu watu wengi hadi sasa wanakabiliwa na tatizo hili, huku idadi kubwa ya watu wengine zaidi wakiwa katika hatari ya kukubwa na ugonjwa huu.

 Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa kimataifa ugonjwa wa kisukari kwa mwaka 2014 uliathiri watu kwa kiwango cha asilimia 9 wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, huku vifo vilivyotokana na ugonjwa huo vilionekana kutokea katika nchi zenye uchumi wa kati na chini kwa asilimia 80.

Sababu kuu za kukithiri kwa maradhi haya yasiyoambukiza ikiwemo kisukari ni pamoja na tabia zinazotokana na hali nzuri ya kiuchumi hasa sehemu za mijini, aina ya vyakula tunavyokula sambamba na ukosefu wa mazoezi.
 
Hayo yote yanaashiria ukubwa wa tatizo hili hivyo kuna haja ya jamii kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa huo kwa kuepukana na vichocheo.
 
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na matatizo ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula. Sukari nyingi mwilini au katika damu, hutokana na kumeng’enywa kwa vyakula vya wanga, kwa mfano ugali, mkate, wali, viazi nk. Wanga inapomeng’enywa inakuwa sukari sahihi iitwayo glukozi ambayo hutumika kuupa mwili nguvu.

Kwa kawaida mwili huwa na kiwango mahususi cha mahitaji ya glukozi, ambapo kiasi fulani cha glukozi hutumika mara moja kuupa mwili nishati na kiasi kingine hubadilishwa na ini na misuli na kuwa glukojeni ambayo hutumika baadaye.

Katika kuhakikisha kwamba kiasi cha glukozi hakipandi au kushuka mwilini kongosho hutoa homoni mbili ambazo ni insulin na glukagoni. 

Mara zote miili yetu huhitaji insulin ili kuweza kutumia sukari tuliyonayo mwilini  vizuri  na endapo kutakuwa na matatizo ya kutengeneza au kutumika kwa insulin sukari mwilini huongezeka haraka na inamaanisha ugonjwa wa sukari upo na dalili huanza kuonekana.

Kwa mujibu wa Dk Abdallah Mandai wa kituo cha tiba asili kiitwacho Mandai Herbalist Clinic anasema kuwa, kuna dalili nyingi za kisukari na miongoni mwa dalili hizo ni mtu kuhisi kiu ya mara kwa mara njaa ya mara kwa mara pamoja na kupungua uzito licha ya kula vizuri.

Dalili nyingine ni kutokwa na jasho jingi, uchovu usioeleweka hata bila kufanya kazi, kizunguzungu, macho kupungua uwezo wake wa kuona na endapo mgonjwa atapata kidonda basi huwa ni kazi sana kupona.

Dk Mandai ambaye pia anatibu ugonjwa huu anasema endapo mtu atapata ugonjwa huo na kutopatiwa tiba inayostahili anaweza kuwa hatarini kwa kupata madhara mengi ambayo huchangiwa na kiwango cha juu cha sukari mwilini.

Mtaalam huyo anabainisha kuwa magonjwa ya moyo, kiharusi, kupungua nguvu za kiume na figo kushindwa kufanya kazi ni miongoni mwa madhara anayoweza kuyapata muathirika wa kisukari.

Hata hivyo, Dk Mandai anasema kuwa “wengi wanasema kisukari hakitibiki ni kweli kwa sababu sukari ukitibu maana unaiondoa hivyo unaweza kumfanya mtu apoteze maisha, lakini ninachofanya mimi natibu kongosho ambayo inafanya kazi ya kuunguza sukari isiyohitajika mwilini na kubakisha sukari ambayo humpa nishati ya kumfanya mtu awe na nguvu”

Dk Mandai anaongeza kuwa “ninachokifanya mimi natibu kongosho kupitia tiba ya mimea. Tiba hii huamsha na kuliimarisha kongosho ili liweze kufanya kazi yake ya kutema insulinna kumfanya mtu arudi katika hali yake ya kawaida”

Mbali na matibabu hayo mtaalam huyo anasema kuwa pia mgonjwa husika hupatiwa darasa la namna ya kutunza mwili wake usishambuliwe na magonjwa kwa kudhibiti ulaji.

Dk Mandai anamalizia kwa kusema kuwa chakula ulacho ndio uzima wako, pia anasema ni vizuri kuzingatia mazoezi na kuepuka kula sukari nyingi pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi na uvutaji wa sigara, lakini pia  kama unasumbuliwa na maradhi sugu ni vizuri kufika kliniki ya Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongalendege jijini Dar es Salaam na utapata tiba sahihi kwa kutumia dawa zitokanazo na mimea na matunda.

No comments:

Post a Comment