Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 22 January 2015

FAHAMU KUHUSU TATIZO LA KISUKARI CHA MIMBAIdadi kubwa ya wanawake nchini hupata ugonjwa wa kisukari cha mimba ujulikanao kitaalam kama ‘gestestional diabetes’.

Kisukari cha mimba kimezidi kushamiri zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Ugonjwa huu umekuwa ukiwaathiri zaidi wanawake wajawazito katika miezi mitatu ya mwanzo wa ujauzito.


Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa, mwaka 2014 kimataifa kiwango cha ugonjwa wa kisukari kwa ujumla kilikuwa ni asilimia 9 kwa miongoni mwa watu wazima wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, huku shirika hilo likieleza kuwa asilimia 80 ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo hutokea kataka nchi zenye uchumi wa chini na wakati.

Dk Mandai anasema, kwa kawaida ugonjwa wa kisukari cha mimba humpata mwanamke mjamzito kipindi cha kuanzia wiki 24 na kuendelea.

Hata hivyo, ugonjwa huu huwa haudumu kwa muda mrefu, kwani hupotea mara baada ya mama mjamzito kujifungua. Pi  kisukari hiki huwa na uwezokano wa kuendelea kwa kubadilika kuelekea katika hatua nyingine tofauti kabisa.

Aidha, Dk Mandai anaeleza kuwa, tatizo hili limekuwa likiwaathiri wanawake walio wengi kutokana na kutokuwa na tabia ya kupima kisukari cha mimba kipindi cha ujauzito. Hali hii huwapelekea kutofahamu hali zao kiafya kuhusu kisukari cha mimba.

Aidha, uchunguzi wa wataalam unaonesha kuwa mjamzito anayeongezeka uzito wa gramu 403.70 kwa wiki yupo hatarini kupata kisukari cha mimba, lakini yule anayeongezeka uzito wa chini ya gramu 272.15 kwa wiki, hayuko hatarini kupata ugonjwa huu.

Sababu za kisukari cha mimba
Kila binadamu huwa na mfumo wa sukari, ambayo ni muhimu mwilini, lakini inategemea sukari ile inaingia kwa kiasi gani mwilini na matumizi yake pia.

Ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi husababisha kongosho kushindwa kufanya kazi yake inayotakiwa. Hali hii husababisha sukari kusambaa mwilini na hivyo kumpelekea mama mjamzito kupata kisukari cha mimba.

Vile vile usugu wa homoni kutumia chembe hai hupelekea tatizo hili, hali hii hutokea kwa watu wenye uzito mkubwa kwa sababu homoni ile inakuwa imezungukwa na mafuta na kufanya uwepo wa mafuta hayo kusababisha ongezeko la baadhi ya vichocheo kama ‘progesterone,’ ‘estrogen’ na ‘castisol’ ambavyo huongeza kiwango cha sukari katika damu na kupelekea ugonjwa huu.

Pia kichocheo cha ‘human placental lactogen’ huzuia ‘insulin’ kufanya kazi kwa ufanisi, hivyo kusababisha kiwango cha ‘insulin’ kuongezeka katika damu.

Mwili unapokuwa umeshindwa kutengeneza ‘insulin’ ya kutosha kwa ajili ya kupambana na ongezeko la sukari katika damu, husababisha kisukari cha mimba.
Mara nyingi hali hii hutokea mimba ikiwa na umri wa miezi mitano au zaidi na huisha wiki sita baada ya mwanamke kujifungua.

Dalili zake.
Kisukari cha mimba kina dalili ambazo kwa kawaida huainishwa kwa vipimo ‘screening’ vinavyochukuliwa na wakati wa ujauzito.

Dk Mandai anabainisha kuhusu dalili za tatizo hili la kisukari cha mimba na kusema kwamba, dalili za kisukari cha mimba ni chache na mara nyingi hazionekani kwa haraka zaidi, hivyo wajawazito wanashauriwa kupima kisukari mara kwa mara.

Miongoni mwa dalili za mwanamke mwenye kisukari cha mimba ni pamoja na kuongezeka uzito siku za mwanzoni mwa mimba, kuwepo historia ya kuwa na kisukari katika familia, kuwahi kujifungua mtoto mwenye uzito mkubwa na mimba kuharibika mara kwa mara.

Dalili nyingine ni mkojo kuwa na sukari, uzito au unene uliokithiri, shinikizo la damu la mda mrefu au umri zaidi ya miaka 35.

Matibabu yake
Kwa kuwa aina hii ya kisukari hutokea wakati wa ujauzito ni bora kumlinda mtoto aliye tumboni kwa kumpatia mama mjamzito ‘insulin’ kwa kufanya hivyo sukari katika damu itaweza kuwa kati ya 4 hadi 8 mm 1/1.

www.dkmandai.com  ambayo ni tovuti (websites) ya Mandai Herbalist Clinic inawapenda sana Watanzania na ndio maana tunatoa elimu hii ya magonjwa mbalimbali kupitia tovuti hii, lakini ikiwa unasumbuliwa na matatizo yoyote ya kiafya ni vizuri ukafika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata tiba sahihi kupitia dawa zetu zisizo na chembe ya kemikali.

No comments:

Post a Comment