Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 19 January 2015

FAHAMU NAMNA AMBAVYO TABIA HUWEZA KUKUSABABISHIA MAGONJWA YA NGONO


Hii ni sehemu ya mdomo ikiwa imeathirika kutokana na magonjwa ya ngono
Ni wazi kwamba watu wengi kwa sasa wamekuwa wakijikuta wakikubwa na maradhi yanayochangiwa na vitendo vya kujihusisha na ngono zisizosalama na wengi wao wamekuwa wakihofia kwenda hospitali kutokana na kuona aibu katika kujielezea kwa matabibu na hivyo kujikuta maradhi hayo yakifikia hatua mbaya zaidi.

Hivyo Dk Mandai hii leo ameona ni vyema kuzungumzia baadhi ya tabia ambazo zinachangia kupelekea maambukizi yatokanayo na magonjwa ya ngono kwa urahisi, hii ni kwasababu hata wahenga wanasema kuwa ni vizuri kujenga ufa kuliko kujenga ukuta, hivyo ni njema ukajua tabia hizo ili kujiepusha nazo.


Miongoni mwa njia moja kubwa inayochangia maambukizi ya magonjwa ya ngono ni kujamiana bila kutumia kinga yaani kondom. Vijana wengi hasa wa jinsia ya kike mara nyingi hukosa ujasiri wa kusisitiza matumizi ya kondom kwa kuhofia kuachwa na wapenzi wao.

Lakini pia wengine hujikuta wakipata maambukizi ya magonjwa ya ngono kwa kufanya ukahaba, kujamiana na wapenzi wengi na kufanya mapenzi ya mdomo, hivyo wengi hujikuta wakiathirika na magonjwa haya ya ngono kwa kuwa vimelea vya magonjwa ya ngono hupatikana kwenye majimaji ya sehemu za siri, hivyo huwa ni rahisi sana kwa mtu mwenye magonjwa hayo kumuambukiza yule anayenyonya sehemu za siri.

Hata hivyo, ni vizuri ikafahamika kuwa baadhi ya vimelea vya magonjwa ya ngono kama kisonono, kaswende na virusi vya UKIMWI hupatikana mdomoni, hivyo mnyonywaji wa sehemu hizo endapo atakuwa na moja ya magonjwa hayo basi huweza kupelekea mnyonyaji kuathirika na hasa endapo kutakuwa na dalili zozote za michubuko.

Mbali na hayo, wengine hujikuta wakijamiana kizembe na kujikuta wakipata maambukizi ya magonjwa ya ngono kwa sababu ya kutazama  filamu za ngono au kushiriki kwenye ngoma za jadi zinazochezwa usiku 'vigodooro' au  kwenda disko na kwenye matamasha, ambapo kuna watu wa aina mbalimbali wanaotumia muda huo kushawishi wenzao kufanya ngono tena zisizosalama.
Magonjwa ya ngono huathiri hata sehemu nyingine za mwili ikiwa ni pamoja na kupata vidonda mdomoni
Hali kadhalika, wengine hupata maradhi haya kutokana na tamaa ya kupata fedha za haraka kutoka kwa watu wenye uwezo mzuri kiuchumi, ambao wengi wao hutumia fedha kama kishawishi au hutoa vitu vya thamani kama vile magari na simu za bei mbaya, nguo, kompyuta mpakato (laptop) na hata nyumba. Hivyo tabia kama hizi pia huchangia zaidi ongezeko la magonjwa haya ya ngono.

Pamoja na hayo, lakini kwa bahati mbaya sana, kuna baadhi ya watu hupata magonjwa haya ya ngono kutokana na kubakwa, kutumia madawa ya kulevya au pombe, hivyo kukosa ufahamu na utashi wa maamuzi na kujikuta wakifanya ngono isiyo salama.

Sambamba na hayo yote ni vizuri pia kufahamu athari za kutotibiwa mapema magonjwa ya ngono
Dk Mandai kutoka kituo bora cha tiba mbadala kiitwacho Mandai Herbalist Clinic kilichopo Mongolandege jijini Dar es Salaam, anasema kuwa  "magonjwa haya yasipotibiwa mapema na kwa usahihi yanaweza kusababisha tatizo la kuziba mirija ya uzazi na kukumbwa na tatizo la mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi au kutozaa kabisa."

Aidha, Dk Mandai anaendelea kueleza kwamba "mgonjwa wa kike asipopata tiba, anaweza kupata maambukizi katika mfuko wa uzazi au kupata magonjwa katika viungo muhimu mwilini au kukumbwa na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, kansa ya kizazi, na hata kupata mabadiliko ya hedhi."

Mbali na wanawake daktari anasema kwa upande wa mwanaume, mgonjwa asipopata tiba mapema anaweza kupata maambukizo katika kokwa za mbegu za uzazi (testis) au kuziba mirija inayopitisha mbegu za uzazi (vas deferens) na hivyo kufanya ashindwe kumpa mimba mwanamke. Hali kadhalika mwanaume huweza kupata matatizo ya kukojoa kwa sababu ya kuziba njia ya mkojo (urethra) sambamba na kupata magonjwa katika sehemu muhimu za mwili kama ubongo, moyo na figo.

Tatizo hili linapokuwa kubwa zaidi bila kupatiwa matibabu sahihi muathirika huweza kupatwa na magonjwa ya moyo, mishipa ya damu na anaweza kukumbwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Lakini Mandai Herbal Clinic inaona  si vyema na haki kukuelezea mambo hayo yote kuhusu tatizo hili la magonjwa ya ngono bila kukuelezea ni namna gani utaweza kutatua tatizo hili yaani tiba.

Ili kukabiliana na tatizo hili unaweza kutumia magome ya muembe kwa kuyachemsha na kisha kunywa asubuhi na jioni kwa muda wa siku 24.

Ushauri.
Ni vizuri ukaacha kusita au kuogopa kwenda hospitali wala kumuonea aibu daktari, kwani magonjwa ya ngono yanatibika. Hivyo, uonapo dalili zinazohusiana na magonjwa hayo ni vyema kumuona daktari haraka sana na ni vyema kuepuka maambukizi ya magonjwa haya kwa kuzingatia kutofanya ngono kabisa na kujiepusha na ulevi ukiwemo wa madawa ya kulevya, lakini pia unaweza sasa kufika Mandai Herbalist Clinic endapo unahisi unatatizo hili na hakika utapatiwa tiba sahihi na utarejea kuwa mzima na mwenye afya bora baada ya kukutana na mtaalam wa tiba mbadala Dk Mandai.

No comments:

Post a Comment