Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 22 January 2015

FAIDA ZA KUTUMIA KITUNGUU SWAUMU KIAFYA

Kitunguu swaumu ni miongoni mwa viungo vinavyotegemewa katika kuongenza ladha nzuri kwenye vyakula mbalimbali,  lakini wakati kiungo hicho kikitegemewa katika kuonogesha vyakula wataalam wa tiba asili wanasema ni kiungo hicho ni dawa endapo kikitumika vizuri.


Miongoni mwa magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kutumia kitunguu swaumu ni pamoja na ugonjwa wa kifua, au mkamba, ambapo mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema kuwa, ugonjwa huo ambao hujitokeza baada ya mifereji inayoingiza hewa mapafuni kupata maambukizi na kusababisha mgonjwa kukohoa kikohozi chenye sauti mara kwa mara, huku kikiambatana na makohozi mazito.

Dk Mandai anasema, ugonjwa mwingine ambao unaweza kutibiwa na kiungo hicho ni kuharisha, hali kadhalika pia husadia kutibumishipa iliyovimba ambayo hujikunja na hivyo kusababisha maumivu makali sana na mara nyingine mishipa hiyo huonekata katika miguu ya watu wa makamo na akina mama wajawazito.

 Pia Dk Mandai anasema kitunguu swaumu ni tiba nzuri ya magonjwa ya ngozi yenye vilenge lenge  (ecsema) ambapo dalili zake ni madoa meupe yenye magamba  (huchunika kama ngozi iliyoungua) mikononi, miguuni, shingoni au usoni kote hutibiwa pia kwa kutumia kitunguu swaumu.

Kitunguu swaumu pia hutibu aina mbalimbali za tambaza kama ya mifu, misuli na viungo pamoja na wale watu wenye matatizo ya kupata choo kwa muda wa siku mbili au zaidi anaweza kutibiwa kwa kutumia kitunguu swaumu.

Aidha, pia inasaidia shida ya pumu na  kubanwa katika mapafu pamoja na kushindwa kupumua ghafla, hali kadhalika hata ukiumwa na ng’e unaweza kusaga kitunguu kisha bandika pale ulipoumwa.

Hizo ni miongoni mwa faida za kitunguu swaumu, lakini unaweza kututembelea kituoni kwetu Mandai Hrbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege kwa kwa ajili ya kupata tiba halisi za mimea.

No comments:

Post a Comment