Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 22 January 2015

GILIGILIANI NI TIBA TOSHA YA MAGONJWA MBALIMBALI
Giligiliani hiki ni kiungo cha kawaida sana, wengi hukitumia kiungo hiki kwa matumizi ya jikoni katika mapishi mbalimbali, kiungo hiki kina harufu nzuri pamoja na ladha ya uchachu kwa mbali.


Mtaalam wa tiba mbadala Dk Abdallah Mandai anasema, majani ya mbegu za mmea huu vyote huweza kutumika kama kiungo cha jikoni, lakini kiungo hiki kina wingi wa vitamin A, B6, C, B12, pia ndani yake kuna wingi wa nadini ya ‘calcium’ chuma na 'magnesium'

Dk Mandai anaendelea kueleza kwamba, giligiliani inasifika kwa kuwa na kinga ya magonjwa mengi, lakini pia kiungo hiki husifika kwa uwezo wake wa kufanya kazi ya usagaji mzuri wa chakula mwilini.

Pia kiungo hiki husaidia kutuliza tumbo na huondoa gesi kwenye utumno mwembamba ambao mara nyingi husababishwa na vyakula tunavyokula, hivyo kiungo hiki hufanya vyema kazi ya kupunguza utoaji wa gesi chafu kwa kiasi kikubwa.

Hali kadhalika, kiungo hiki husaidia kuzuia magonjwa ya tumbo yanayotokana na bacteria aina ya ‘salmonella’ moja ya magonjwa haya ni kuumwa tumbo na kuhara, pia huzuia ugonjwa wa ‘Urinary Tract Infection (UTI).’

Pamoja na kuwa kiungo hiki kimeonekana kuweza kusaidia katika magonjwa mbalimbali, lakini pia huweza kusaidia kuzuia kutapika pamoja na hali ya kuvurugika kwa tumbo.

Mbali na faida hizo za giligiliani, pia husaidia kushusha sukari kwenye damu (lower blood sugar) na hupunguza  pia ‘cholesterol’ mbaya mwilini. Pia ni chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zinazohitajika mwilini, ili kuwezesha usagaji mzuri wa chakula (dietary fiber) na inawafaa sana wanawake ambao hupata hedhi nzito.

Sambamba na hayo, pia kiungo hiki husaidia kuondosha maumivu  na muwasho pamoja na uvimbe. Hali kadhalika huweza kusaidia kuondoa chunusi na madoa kwenye ngozi.

Jinsi ya kuandaa giligiliani katika njia mbalimbali ili kuitumia kama dawa.
Kuondoa hedhi nzito.
Chemsha kijiko cha mbegu za giligiliani na maji vikombe viwili, kisha chuja na uongeze sukari kidogo na unywe ikiwa ya moto au uvuguvugu.
 
Kuondoa maumivu (inflammation)
Chemsha kijiko kimoja cha chai cha mbegu za giligiliani zilizosagwa na maji kikombe kimoja, naada ya hapo chuja kisha unywe ikiwa ya uvuguvugu.

Kushusha sukari na lehemu
Kunywa chai ya giligiliani (mbegu) mara kwa mara, pia tumia mbegu na majani ya giligiliani kwa wingi kwenye chakula chako.

Kutibu kuhara damu
Changanya  vijiko viwili vya chai vya maji ya giligiliani na kikombe kimoja cha maziwa fresh, ambayo hayajatolewa krimu, lakini pia chai ya giligiliani (mbegu) husaidia kuondoa au kutuliza acid tumboni, hivyo matumizi ya mara kwa mara ya vyakula ambavyo ni tiba husaidia kuupa mwili nafasi ya nzuri ya kuvuna virutubisho na kupambana na magonjwa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment