Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 19 January 2015

HOMA YA MAPAFU NI TISHIO KWA WATOTOWatoto ni miongoni mwa waathirika ambao nao pia hukabiliwa na tatizo la homa ya mapafu maarufu kama nimonia (Pneumonia). ambapo tatizo hili limekuwa likichangia kusababisha vifo vya watoto wengi duniani kote.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa maradhi haya ya homa ya mapafu mnamo mwaka 2013 yalisababisha vifo vya watoto wapatao 935,000 wenye umri chini ya miaka mitano. Huku ikielezwa kuwa asilimia 15 ya vifo vya watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano ulimwengunu huchangiwa na maradhi haya.


Kutoka  na ukubwa wa tatizo hili Shirika la Afya Duniani WHO liliamua kutenga siku ya Novemba 12 iwe siku rasmi ya homa ya mapafu duniani ikiwa na lengo la kuwajuza walimwengu juu ya maradhi hayo na namna ya kuwahamasisha jinsi ya kujikinga na kuyatibu pia.

Dk Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic ambacho ni kituo cha tiba mbadala kilichopo Mongolandege jijini Dar es Salaama anasema kwamba Homa hii ya mapafu ni aina ya maambukizi yanayoathiri mapafu, huku akisema kuwa ni vyema  tukatambua kwamba mapafu yanajumuisha mirija mikubwa ya hewa inayoitwa 'bronch'  ambayo hugawanyika na kufanya mirija midogo zaidi ya hewa inayojulikana kama 'bronchioles' ambayo nayo hutengeneza vifuko vidogo vidogo vya hewa vinavyoitwa 'alveoli'.

Vifuko hivyo vidogo vya hewa huwa na mishipa ya kupitisha damu ambayo husaidia kuchuja na kusafirisha hewa safi ya oksijeni tunayovuta kuingia kwenye damu, huku hewa chafu ya kabonidayoksaidi huondolewa kwenye damu na kuingizwa kwenye mapafu tayari kwa ajili ya kutolewa nje ya mwili.

Kwa kawaida vifuko hivi vidogo hujaa hewa muda wote tayari kusafirishwa, sasa pale inapotokea mtu akapata homa ya mapafu vifuko hivyo hujaa maji au usaha na hivyo kuathiri upitishaji wa hewa safi kwenye damu na kusababisha tatizo la kupumua.

Hivyo Mandai Herbalist Clinic inapenda kutoa wito kwa wazazi kujenga tabia ya kuwafanyia utafiti wa kiafya watoto wao mara kwa mara ili kutambua matatizo ambayo mara nyingi ni vigumu kuonekana mara moja likiwemo hili la homa ya mapafu.

No comments:

Post a Comment