Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 26 January 2015

ISHARA MUHIMU ZA UJAUZITO NA MAMBO YA KUZINGATIWA WAKATI WA HALI HIYO


Mimba ni mwanzo wa maisha mapya, huanza na utungaji na kuendelea na ukuaji wa kijusi mpaka kujifungua. Mimba ni mfumo wa kisaikolojia wa kawaida katika ukuaji wa kiumbe.

 Kumekuwa na njia nyingi kama vipimo na ishara za kudhibitisha kuwa mwanamke fulani ni mjamzito, miongoni mwa ishara zinazoashiria mwanamke ni mjamzito ni pamoja na kukoma kwa hedhi (amenorrhea).

Mwanamke aliyefikia wakati wa kupata mtoto ni lazima apate mzunguko wa siku (hedhi), lakini pindi mimba inapotungwa mzunguko huo hukoma ili kupisha utaratibu wa ukuaji wa kijusi kuendelea.

Ishara nyingine ni kichefuchefu na kutapika, hali hii huambatana na kichwa kuuma pamoja na kizunguzungu. Pia pindi mimba unapotunga inaweza kutokea homa za asubuhi. Hii hutokea sana iwapo ni mimba ya kwanza.

Hali kadhalika, mwanamke hupata mabadiliko kwenye matiti, kwani wakati wa ujauzito matiti huongezeka ukubwa na huwa na hisia kali.

Mbali na ishara hizo, ishara nyingine ni pale ambapo tumbo la mwanamke linapoanza kujitokeza hususani kuanzia miezi mitatu na hii huwa ni ishara kwa watu wengine kutambua hali halisi. Miezi mitano, mtoto huanza kucheza tumboni kuashiria kuwa kuna kiumbe tayari.

Wakati wa ujauzito, mama huwa na mabadiliko makubwa kwa ndani, huku hali hiyo ikiathiri mifumo mingine, kwa mfano mfumo wa uyeyusho wa chakula tumboni na huchangia sana kumfanya mama kujihisi  hamu ya kula zaidi.

Aidha, katika hali ya ujauzito mama huweza kupata matatizo ya mdomo na meno hii ni kwa sababu ya kupungua kwa ‘fluoride,’ lakini tatizo hili linazuilika. Kuvimba kwa fizi hujitokeza sana sambamba na kuvuja damu wakati wa kupiga mswaki, mama mjamzito akiona na dalili hizi anashauriwa kumwona daktari wa meno.

Hali kadhalika, mzunguko wa damu na mfumo wa upumuaji wa mama mjamzito hubadilika, pia mama huwa na hatari ya kupata magonjwa mengine huongezeka. Huku kasi ya damu ikiongezeka kati ya mwezi wa pili au watatu wakati wa ujauzito, hadi kufikia wiki ya 35 ongezeko hili hufikia kati ya asilimia 25 hadi 40.

Mambo muhimu ya kuzingatia kwa mamamjamzito.

Kula mlo kamili
Mama mjamzito ni vizuri ukala mlo kamili na ni vizuri kula chakula cha asili, kilichoandaliwa katika hali ya usafi na rahisi na chenye virutubisho vyake vyote muhimu.


Mapumziko
Mama anashauriwa kulala masaa 9 kwa siku badala ya masaa nane ambayo hushauriwa na wataalam kwa watu wa hali ya kawaida.


Usafi
Mamamjamzito unatakiwa kuwa msafi wa kuanzia katika mavazi yako, mwili, mikono na ni vizuri ukawa na kawaida ya kumuona daktari mara kwa mara.

Mazoezi
Mazoezi kwa mamamjamzito ni muhim sana, hivyo ukiwa wakati wa ujauzito ni vizuri ukafanya mazoezi mepesi, mfano  tembea japo saa 1 kwa siku.

Sambamba na hayo, mamamjamzito unaweza kuwa na wakati wa kusoma vijarida, magazeti, vitabu vyenye hadithi nzuri au kusikiliza muziki laini na mzuri. Epuka habari za huzuni, makelele, kuchoka, safari zisizo na umuhimu, sigara na pombe.

Hayo ni baadhi ya mambo muhimu juu ya ishara za ujauzito pamoja na mambo ya kuzingatiwa kwa mamamjamzito. Unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic na kukutana na Dk Abdallah Mandai kwa ajili ya kuweka afya yako kuwa bora zaidi kupitia dawa zake zitokanazo na mimea na matunda na zisizo na kemikali pia. 

No comments:

Post a Comment