Thursday, 29 January 2015

JIFUNZE NAMNA YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA PUMU


Pumu ni miongoni mwa magonjwa sugu ya hewa yanayosumbua idadi kubwa ya watu duniani na hasa watoto, huku idadi ya wanaokabiliwa na tatizo hili ikionekana kuongezeka siku hadi siku.
Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anaanza  kwa kusema kuwa “kwa kawaida binadamu anapovuta pumzi/ hewa huenda kwenye mdomo au pua kupitia katika mirija ya hewa na kusafiri hadi kwenye mapafu katika mlolongo huu wa usafirishaji hewa kupitia mirija yake , tatizo la pumu huibuka pindi njia hizo zinapoingiliwa na kitu kutoka nje na kusababisha ugumu katika upumuaji”

Anaeleza hali hiyo ya tatizo la upumuaji hujitokeza kutokana na kubana kwa mirija ya hewa kunakotokana na kubadilika kwa utendaji kazi wa viungo hivyo kunakosababishwa na kuchochewa na kitu kilichoingia kutokea nje inawezekana ni hewa chafu, vumbi au chavua ambacho huchochea kuundwa kwa sumu katika mwili wa mhusika, lakini kunauwezekano wa kitu hicho hicho kutokuwa na madhara kwa mtu mwingine endapo kitaingia katika mirija yake  ya hewa  anapopumua. Hali hiyo ndiyo hujulikana kama mzio au (allergy).

Aidha, mtaalam huyo anasema kwa kiasi kikubwa tatizo hili la pumu hupatikana kwa njia ya kurithi na hasa kwa wale watu wenye matatizo ya mzio (allergy)
Ugonjwa wa pumu umegawanyika katika makundi mawili, ambapo aina ya kwanza ya ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kurithi hasa kwa wale watu wenye matatizo ya mzio (allergy) hivyo aina hii hufahamika kwa jina la ‘allergic asthma’ ambayo ipo sana kwenye nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania.

Aina hii ya kwanza ya pumu kwa sehemu kubwa husababishwa na chavua (pollen), ukungu (fog), wanyama pamoja na chembechembe za vumbi n.k, lakini pia aina hii ya pumu huweza kuingia mwilini kupitia kitu chochote kilicholiwa mfano samaki. nk.

Manyoya ya wanyama wa kufungwa pia ni hatari kwa mtu mwenye pumu kwani husababisha kuchochea shambulizi la pumu ya mzio (allergy) au ‘allergic ‘asthma’
Aina ya pili ya ugonjwa huu wa pumu hufahamika kwa jina la ‘non allergic asthma’ hii haitokani na matatizo ya mizio au kurithi kutoka kizazi kilichopita, hivyo huweza kumpata mtu yeyote kwani aina hii husababishwa na hewa kavu, baridi kali, mazoezi, moshi, manukato yenye harufu kali, msongo wa mawazo, nk.

Dalili za ugonjwa huu hazitofautiani kutokana na vyanzo vyake bali zote hufanana na hujitokeza sawa katika mwili wa mwanadamu na miongoni mwa dalili hzio ni pamoja na kifua kubana, kikohozi kikavu, mapigo ya moyo kwenda mbio, kukosa hewa ya kutosha kwenye mirija, kuhisi baridi.

Mtu mwenyea tatizo la pumu hushauriwa mara anapojigundua kuwa anashida hii anapaswa kumuona daktari ili kufanyiwa vipimo zaidi vya kina na kugundua chanzo cha tatizo lake na jinsi ya kukabiliana nalo.

Hata hivyo, Dk Mandai anasema unaweza kuepukana na maradhi haya kwa kuepuka kukaa maeneo yanayochangia shambulizi la pumu kwako kutokana na maelezo ya daktari wako, epuka pia vipodozi vya manukano yenye harufu kali ambayo  pia kula vyakula vyenye asili ya mboga za majani kama vile nyanya, bilinganya, maharage, matango na vyote vyenye asili hiyo.

Kama unngependa kuonana na kuzungumza vizuri na Dk Abdallah Mandai kuhusu tatizo la la kiafya fika  sasa Mandai Herbalist Clinic kituoni kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam


No comments:

Post a Comment