Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 30 January 2015

KABICHI KAMA TIBA YA MAGONJWA NA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME
Kabichi ni mboga inayopatikana maeneo mengi hapa duniani, lakini tu hutofautiana rangi kutoka kabichi ya eneo moja na jingine pia ni dawa.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema kwamba, mboga hii wengi huitumia katika maisha ya kila siku tunayoishi, isipokuwa watu wengi hawafahamu kuwa ni dawa ya magonjwa mbalimbali pale inapotumika vizuri kwani huweza kusaidia matatizo ya kikohozi sugu pamoja na kusaidia wale wenye matatizo ya usagaji wa chakula.

Aidha, mtaalam huyo anasema kuwa, kabichi pia husaidia kutibu minyoo, pumu, pamoja na junjua (warts), na pia anasema huweza kutumika kama kisafisha tumbo kwa kumsaidia mtu kuhamasisha kuharisha.

Dk Mandai anaendelea kufafanua kuwa mboga hii huwasaidia wale wenye matatizo ya pumu na inapunguza unene, lakini pia ni kibandiko kizuri juu ya vidonda, uvimbe na penye maumivu.

Kabichi huwa na rangi tofauti miongoni mwa rangi hizo ni pamoja na kijani na zambarau   
Hali kadhalika, kuna baadhi ya watu ambao ni wanywaji wazuri wa pombe, lakini wangependa kuachana na tabia hiyo na wameshindwa, lakini hapa mtaalam huyo anasema kabichi huweza kuvunja tabia ya kuzoea ulevi, ambapo mhusika atapaswa kunywa juisi ya kabichi kwa kutumia kijiko kimoja kikubwa kila saa.


Mbali na hayo, pia kabichi husaidi kukuweka katika muonekano mzuri na hasa katika masuala ya utunzaji wa nywele, ambapo katika suala hili mhusika atapaswa kuoshea nywele zake juisi ya kabichi mara mbili kwa kutwa.

Pamoja na hayo pia kabichi huondoa vijipele juu ya ngozi na inatibu vidonda vya tumbo pia ni kibandiko kizuri juu ya vidonda, uvimbe na sehemu zenye maumivu.

Hata hivyo, pamoja na faida hizo za kabichi Dk Mandai anatoa onyo kuwa matumizi ya kabichi kupita kiasi si mazuri kwa sababu huhamasisha shida ya koo na kukaribisha goita.

Acha kuteseka na magonjwa anza sasa kutumia mimea na matunda kwa kuimarisha afya yako au fika Mandai Herbalist Clinic Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata matibabu sahihi ya magonjwa yanayokusumbua kwa kutumia dawa asili zinazotokana na mimea na matunda.

No comments:

Post a Comment