Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 28 January 2015

KITUNGUU MAJI KIUNGO CHA JIKONI CHENYE UWEZO WA KUOKOA MAISHA YAKO
Kitunguu maji ni moja ya kiungo ambacho hutumiwa sana na binadam karibu kila siku, hasa katika shughuli za jikoni, lakini kiungo hiki pia ni tiba kwa matatizo ya afya zetu.


Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anaeleza kwamba, unapotwanga gramu thelathini ikiwa na pilipili manga saba na kisha kumpatia mgonjwa mwenye tatizo la kutapika na kujisikia vibaya pamoja na kuharisha humsaidia sana kupona.

Aidha, Dk Mandai anaendelea kueleza kwamba kwa wale wenye shida ya haja ndogo (mkojo) kuuma anaweza kuponda kiasi cha gramu sita ya vitunguu na baadaye kuchemsha katika nusu lita ya maji na kuiacha ichemke hadi pale itakapo pungua nusu ya ule ujazo wote kisha apatiwe mgonjwa anywe.

Pia mtaalam huyo anabainisha kwamba matone ya maji ya kitunguu huweza kusaidia kuwa dawa ya sikio na kusaidia kuondoa milio yote ya sikioni na tatizo hilo litaacha.

Matatizo mengine yanayoweza kutatuliwa na kiungo hiki ni pamoja na kikohozi, vidonda vya tumbo, ngozi, figo pamoja na tumbo.

Dk Mandai anasema kuwa, kwa tatizo la kikohozi kinachotakiwa kufanyika ni kuchukuwa kitunguu maji kimoja kikubwa na ukikate kate kwenye maji kisha chemsha maji hayo dakiaka tano na baadaye mgonjwa anywe kijiko kikubwa kimoja kutwa mara tatu yaani asubuhi mchana na jioni.   

Endapo unasumbuliwa na tatizo lolote kiafya ni vizuri ukafika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege na kukutana na Dk Abdallah Mandai na utapata huduma sahihi kwa ajili ya kurejesha afya yako katika hali nzuri tena kwa kutumia dawa asili zitokanazo na mimea na matunda.

No comments:

Post a Comment