Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 30 January 2015

KUHISI KIUNGULIA NI ISHARA YA UGONJWA WA SARATANI
Imeelezwa kuwa kuhisi kiungulia kwa zaidi ya siku kadhaa inaweza kuwa ni ishara ya kuwepo kwa ugonjwa wa saratani.

Hii ni kwa mujibu wa madaktari kutoka nchini Uingereza mjini Devon, ambao wanaunga mkono kampeni mpya inayowaagiza raia kuwatembelea madaktari wao iwapo wanahisi kuwa na kiungulia kwa siku kadhaa kwa kuwa huenda ikawa ni ishara ya ugonjwa wa saratani.

Kampeni hiyo inayofanywa na Idara ya Afya ya Umma nchini Uingereza inasema watu sita kati ya kumi hawajui kwamba kiungulia huenda kikawa ni ishara ya ugonjwa wa saratani, huku ikiongeza kuwa karibia nusu ya watu hutembelea madaktari wao iwapo wanaugua kiungulia kwa wiki tatu ama zaidi.

Taarifa zinasema kuwa zaidi ya watu 10,000 hufariki kutokana na saratani ya tumbo au ile ya koromeo kila mwaka huko nchini Uingereza ambayo ni sawa na watu 28 kila siku.
 
Aidha, daktari Tom Debenham kutoka Devon na mkuu wa kliniki za kaskazini, mashariki na magharibi mwa Devon anasema kuwa, watu wanafaa kuelezwa kuhusu uhusiano kati ya kiungulia na saratani.

 ''Iwapo unahisi kiungulia kila mara, nenda ukamuone daktari , hata iwapo unatumia dawa na unahisi zinakusaidia,'' anasema Dk Debenham.

Pamoja na hayo daktari huyo anaongeza kwamba ''huenda si kitu chochote hatari lakini iwapo ni saratani kuigundua mapema inakuwa rahisi kuitibu.''

Pamoja na hayo watu pia wameagizwa kujenga tabia ya kuwatembelea madaktari wao iwapo kila wanapomeza chakula wanahisi kwamba chakula kinazuiliwa katika koromeo.

No comments:

Post a Comment