Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 20 January 2015

KUTANA NA DK MANDAI HAPA AKIELEZEA KUHUSU MAAMBUKIZI YA FANGASI SEHEMU ZA SIRIDk Mandai akionesha baadhi ya dawa zinazopatikana Mandai Herbalist Clinic

Maambukizi ya fangasi sehemu za siri ni miongoni mwa matatizo yanayowasumbua wengi katika jamii na hasa wanawake, ambapo inakadiriwa kuwa asilimia 75 ya wanawake duniani hupata maambukizi haya.


Ni ukweli usiopingika kwamba wanawake wengi wamekuwa wakihitaji maelezo zaidi  juu ya tatizo hili huku wakidai kuwa wanasumbuliwa na ugonjwa huo.
Ni kweli fangasi husumbua sana wanawake zaidi ya wanaume na kuwashwa sehemu za siri ni dalili ya kuwa na ‘candida albicans.’

Mandai Herbalist Clinic inakujuza kwamba miongoni mwa dalili za tatizo hili ni pamoja na kuwashwa sehemu za siri za mwanamke na kwa upande wa wanaume huvimba uume hasa sehemu ya mbele na kuwa na rangirangi nyeupe sehemu ya juu ya uume, huku dalili nyingine ikiwa ni pamoja na mgonjwa kuwa na vidonda vidogo kwenye uume.

Endapo utakuwa na dalili hizo unashauriwa kwenda kumuona daktari kwa lengo la kufanyiwa uchunguzi ambapo daktari ataweza kufanya uchunguzi sehemu za siri kitaalam huitwa ‘PV exam.’

Hali kadhalika daktari pia atahitaji kuchunguza endapo kuna uchafu wowote unaotoka na kuangalia wingi wake, rangi, harufu yake, lakini pia mgonjwa anashauriwa kuwa huru kumsimulia daktari tatizo lake.

Mbali na hayo, mgonjwa atachunguzwa kama ana mitoki sehemu za siri na daktari ataangalia shingo ya kizazi na sehemu ya haja kubwa kama kuna bawasira (hemorrhoids) n.k

Mgonjwa anaweza kufanyiwa vipimo vya mkojo yaani ‘urinalysis’ na kuangaliwa kama ana dalili za magonjwa mengine kama vile kisukari, VVU/UKIMWI, ugonjwa wa kuvimba tezi la koo au saratani ya tezi koo yaani ‘thyroid cancer’ n.k.

Mandai Herbalist Clinic inapenda kukushauri mara uonapo dalili za tatizo hili ni vizuri ukawaona wataalam ili uweze kufanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa tiba sahihi, lakini pia endapo kama baada ya matibabu tatizo likawa linaendelea basi ni vizuri kwenda kumuona tena daktari ili kupata matibabu zaidi. Hali kadahalika unaweza kufika kituoni kwetu kilichopo Mongolandege jijini Dar es Salaam ambapo pia unaweza kupata suluhisho la tatizo lako.

No comments:

Post a Comment