Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 23 January 2015

MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA HEWA YAELEZWA KUSABABISHA KIFO CHA MFALME WA SAUDIAHayati Mfalme Abdullah


Taarifa zilizoifikia BBC saa chache zilizopita zinaeleza kuwa, mfalme wa Saudia Abdullah bin Abdulaziz amefariki dunia akiwa hospitalini.


Taarifa hizo zinaarifu kuwa, tamko la kifo cha mfalme huyo zilitolewa na kaka wa mfalme huyo aitwaye, Salman, ambaye naye aliwahi kuwa mfalme.

Aidha, inaelezwa kuwa kabla ya tamko hilo Television ya Taifa la Saudia lilikatiza matangazo yake na kuweka nyimbo za quraan, ikiwa kama ishara ya kifo cha kiongozi wa juu wa ufalme.

King Abdullah, amefariki dunia akiwa na miaka 90, alilazwa hospitalini kwa wiki kadhaa tangu mwezi Disemba mwaka jana kutokana na maambukizi kwenye njia ya hewa.

Mbali na hayo, taarifa zinaeleza kuwa mfalme huyo aliingia madarakani mwaka 2005, lakini alikuwa ni dhaifu na mwenye kushambuliwa na maradhi mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment