Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 23 January 2015

MAJARIBIO YA CHANJO YA EBOLA YATAANZIA NCHINI LIBERIA
Chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola inatarajia kufikishwa nchini Liberia. Ikiwa ni mara ya kwanza kwa chanjo hiyo kupelekwa kwenye nchi iliyoathiriwa zaidi na Ebola.


Lakini pamoja na kutarajiwa kupelekwa kwa chanjo hiyo, wataalam wamekuwa wakisema kwamba, wakati huu maambukizi ya Ebola yamepungua, hivyo itakuwa ni vigumu kubaini kama chanjo hiyo inatoa kinga dhidi ya virusi vya ugonjwa huo.

Chanjo hiyo iliyotengenezwa na Kampuni moja ya nchini Uingereza, GlaxoSmithKline (GSK) na Taasisi ya Kitaifa ya Afya nchini Marekani, GSK imesema ndege iliyobeba dozi za awali takriban 300 za chanjo hiyo inatarajiwa kufika hii leo Ijumaa mjini Monrovia.

Aidha, katika majaribio ya chanjo hiyo wanasayansi wamelenga kuwahusisha watu watakaojitolea takribani 30,000 katika majaribio hayo wakiwemo wafanyakazi wa afya, huku wakisema kwamba endapo taratibu zote zitafuatwa, basi watu 10,000 watapatiwa chanjo hiyo ya GSK.

Lakini mbali na hayo, inaelezwa kuwa idadi hiyo hiyo ya watu pia watapata chanjo aina ya Placedo, na wengine 10,000 chanjo nyingine ya majaribio kisha  matokeo yatalinganishwa ili kubaini kama kuna chanjo yoyote kati ya hizo imefanya kazi dhidi ya virusi vya Ebola.

Majaribio kama hayo tayari yalishafanyika kwa wafanyakazi wa afya 200 waliojitolea nchini Uingereza, Marekani, Switerland na Mali. Huku Shirika hilo laGSK likisema chanjo hizo zimeleta matokeo chanya.

Hata hivyo, kampuni hiyo inasisitiza kuwa chanjo hiyo bado iko katika uboreshwaji na Shirika la Afya duniani (WHO) na wakaguzi wengine wanakazi ya kuhakikisha kuwa wanajiridhisha kuhusu ubora na usalama wake kabla ya kampeni za matumizi ya kinga hiyo .

Ifahamike kwamba chanjo  hizo pia zimepangwa nchini Guinea, Liberia Sierra Leone miezi kadhaa ijayo.

Chanzo:BBC Swahili

No comments:

Post a Comment