Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 26 January 2015

MATATIZO YA HOMA YA MAPAFU KWA WATOTOWiki iliyopita kupitia tovuti hii tulianza kuelezea tatizo la homa ya mapafu kwa watoto ambayo kitaalam huitwa ‘Pneumonia’ au ‘Nimonia’, hivyo leo tunapenda kuendelea kwa daktari kuelezea zaidi juu ya tatizo hili la homa ya mapafu kwa watoto.


Dk Abdallah Mandai anasema kuna aina kadhaa ya vimelea ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi katika mapafu. Vimelea hivi hujumuisha bakteria, virusi, ‘Parasaiti’ na fangasi.

Mtaalam huyo anaeleza kuwa, vimelea hivi hushambulia mwili wa binadam kulingana na umri na kinga ya mwili ya mtu husika. Kwa mfano, bakteria wanaosababisha ugonjwa huo kwa watoto wachanga ni tofauti na wale wanaosababisha ugonjwa huo kwa watoto wakubwa.

Baadhi ya vimelea wa bacteria wanaoshambulia watoto ni pamoja na ‘Streptococcus Pneumonia,’ ambao ni aina ya bakteria wanaoongoza kusababisha homa ya mapafu kwa watoto.

Wapo pia ‘Haemophilus Influenza’ aina ya Hib, ambao ni aina ya pili ya ya bakteria walio maarufu kwa kusababisha ugonjwa wa homa ya mapafu kwa watoto, huku ‘Staphylococcus Aureus’ ni aina nyingine ya bakteria ambao hushambulia zaidi ya watoto wachanga.

Aidha, kwa upande wa virusi aina ya ‘respiratory syncytial virus’ ndiyo wanaoongoza kwa kusababisha homa ya mapafu kwa watoto.

Vimelea wengine ni wale wa ‘Pneumocystis Jiroveci’ ambao kwa sasa huwekwa kwenye kundi la ‘Parasait’ ni maarufu zaidi miongoni mwa parasaiti wanaosababisha homa ya mapafu kwa watoto wenye upungufu wa kinga mwilini hususani wenye virusi vya UKIMWI.

Sambamba na aina hizo pia aina nyingine za bakteria ambao hushambulia zaidi watoto ni ‘Mycoplasma Pheumonia’ na ‘Chlamydia Pneumonia.’

Baada ya kufahamu aina hizi za vimelea mbalimbali wanaosababisha ugonjwa wa homa hii ya mapafu kwa watoto napenda kukuahidi kuwa Dk Mandai kupitia kituo cha Mandai Herbalist Clinic wiki ijayo atakuletea muendelezo wa ugonjwa huu na tutaangalia jinsi homa ya mapafu inavyoenezwa, lakini endapo unatatizo lolote kiafya unaweza fika kituoni Mandai Herbalist Clinic kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhu la tatizo lako.

No comments:

Post a Comment