Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Friday, 23 January 2015

MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA HUWATESA WANAWAKE, HIVYO FAHAMU NAMNA YA KUEPUKANA NAYO
Maumivu wakati wa tendo la ndoa huwakabili baadhi ya watu na kusababisha baadhi yao kulichukie kabisa tendo hilo na hata kukosa mhuemko wa kushiriki tendo hilo.

Mtaalam wa tiba mbadala Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema, mara nyingi maumivu yanayotokea mwanzoni wakati wa tendo la ndoa halafu yanapotea baadaye, hali hii husababishwa na upungufu wa ute unaoilainisha njia ya uzazi na mara nyingi hutokana na maandalizi hafifu wakati wa tendo husika.

Lakini pia Dk Mandai anasema licha ya sababu hiyo pia tatizo hili wakati mwingine hutokea baada ya mwanamke kumeza dawa zinazohusisha majimaji ukeni kama vile dawa za kuzuia uzio na nyinginezo.

Adha, tatizo la maumivu wakati wa tendo la ndoa huweza kusababishwa na athari za kisaikolojia anazokuwa nazo mwanamke. Mfano, kama mwanamke aliwahi kubakwa au kufanyiwa vitendo viovu mara nyingi mwanamke wa aina hii huweza kuwa na hali ya kutohisi hamu ya tendo la ndoa.

Wanawake wenye uwezekano wa kukumbwa na tatizo hili
Dk Mandai anasema, tatizo hili huweza kuwapata wanawake ambao muda wao wa kupata hedhi umekoma, hii ni kwa sababu baadhi ya vichocheo (homoni) vinavyochochea kutolewa kwa majimaji ili kulainisha njia ya uzazi hupungua kwenye damu, huku wengine wakiwa ni wale wenye matatizo ya maambukizi ya magonjwa katika viungo vyao vya uzazi hususani magonjwa ya zinaa.

Pia maambukizi kwenye njia ya mkojo hasa kwenye kibofu cha mkojo huleta maumivu wakati wa tendo la ndoa, hali kadhalika na wale wanawake wenye matatizo sugu ya kukosa choo wao nao wanauwezekano mkubwa wa kupata maumivu haya.

Mbali na sababu hizo pia endapo mwanamke atafanya tendo la ndoa kipindi kifupi mara baada ya kujifungua huweza kupata maumivu wakati wa tendo hilo. Hii ni kwasababu mwanamke anapojifungua, viungo vyake vya uzazi huchukua muda mrefu hadi kurudi katika hali yake ya kawaida, hivyo basi anaposhiriki tendo la ndoa muda mfupi baada ya kujifungua kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kuhisi maumivu. Pia tatizo hili huwapata wanawake waliojifungua kwa kuongezwa njia ya uzazi.

Maumivu kwa wanaume
Dk Mandai anaeleza kuwa hata wanaume huweza kupatwa maumivu ya aina hii wakati wa tendo lenyewe au wakati wa kutoa mbegu. Pia maumivu haya husababishwa na maambukizi au vidonda kwenye ‘gland,’ ambavyo huruhusu mbegu kutoka ‘prostate gland’

Aidha, maumivu kwa wanaume pia huweza kusababishwa na maambukizi kwenye ngozi inayofunika uume na magonjwa ya malengelenge na baadhi ya magonjwa ya zinaa. Hizo ni baadhi ya sababu, ambazo mara kwa mara husababisha tatizo hili.

Athari                                                   
Ni jambo la muhimu kwenda hospitali unapokuwa na tatizo hili kuliko kukaa kimya, jitahidi kumuelezea daktari namna maumivu hayo yanavyokutokea. Mfano utapaswa kumueleleza daktari maumivu unayoyapata yana muda gani na hutokea baada ya tendo lenyewe au ni tofauti. Hivyo daktari atafahamu ni dawa gani akupatie.

Magonjwa ya zinaa yanachangia tatizo hili, hivyo ni vyema kwenda na mwenza wako mkachunguzwe na kutibiwa wote na mara nyingi tiba hufanyika kwa kutegemea sababu iliyosababishwa na unaweza kumuona mtaalam wa matatizo ya kisaikolojia kwa msaada zaidi, wale wenye tatizo la kisaikolojia wanashauriwa kumuona daktari wa matatizo ya kisaikolojia kwa msaada zaidi.

Kinga
Dk Mandai anasema, ni muhimu kuzingatia usafi kwani hupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya maambukizo. Huku akiongeza kwamba kila mtu anatakiwa kumuandaa mwenzake wakati wa tendo hilo jambo ambalo husaidia maji ya kulainisha njia ya uzazi yatoke ya kutosha. 

Kwa wanawake hakikisha haushiriki tendo la ndoa mara baada ya kujifungua ni vizuri ukasubiri  angalau baada ya wiki sita.

Tiba
Dk Mandai anakujuza kwamba, unaweza kuchukua kokwa la embe  kisha ukaponda ponda na baadaye kausha au twanga, kisha utapata unga wake ambao utatumia katika uji mwepesi 1x3 kwa muda wa siku 14 hii husaidi katika tatizo hilo. 

Mandai Herbalist Clinic tunapatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam unaweza kufika katika kliniki yetu na kupata huduma za matibabu zenye kutumia tiba asili za mimea zisizo na kemikali na ukapona kabisa.

No comments:

Post a Comment