Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 24 January 2015

MIUJIZA YA MTI WA MLONGE KATIKA KUTIBU MAGONJWA


Hapa nchini kuna miti ya aina mbalimbali ikiwemo ile inayotambulika na jamii kutokana na umaarufu na ipo mingine ambayo pia haifahamiki kabisa.


Mfano wa baadhi ya miti ambayo inafahamika kiasi kwamba hata ukiitaja katika kundi la watu basi ni lazima asilimia kubwa watakuwa wanaifahamu ni pamoja na mti wa muarobaini na mbuyu, ambayo imekuwa ikifahamika kama miti dawa na imekuwa ni msaada mkubwa kwa wale ambao hufahamu matumizi yake.

Miti mingine ambayo pia ni dawa ni ile ya aina ya Miyombo ambayo pale inapokauka huweza kutumika kama kuni hii ni kutokana na miti hiyo kuaminika kuwa kuni zake hutoa mkaa mzito na wenye kudumu kwa muda mrefu.

Pamoja na faida na umaarufu wa miti hiyo, lakini hapa Dk Abdallah Mandai anabainisha mti mwingine ambao umekuwa na historia ndefu katika masuala ya tiba.

Dk Mandai anasema mti huo ni mti wa mlonge ambao pia ameufanyia utafiti kwa muda mrefu na ni tiba nzuri kwa magonjwa mengi ya binadamu.

"Tafiti zangu ama vyanzo vikubwa vya utabibu wa leo vinakubaliana kwamba huu ndiyo ule mti ambao Mussa alioneshwa na Bwana katika Kitabu cha Kutoka sura ya 15 na uliotumika katika kuyatibu maji ya pale Mara" anasema

Anafafanua kuwa, licha ya mti huo kutibu magonjwa mbalimbali, mlonge pia ni dawa ya inayowekwa kwenye maji na kuua wadudu na kusafisha maji ya kunywa.

"Funga fundo dogo la unga wa majani ya mlonge katika kitambaa safi, tumbukiza kwenye ndoo ya maji, utakuwa umeua wadudu na kuyasafisha maji yote" anasema Dk Mandai.

Hata hivyo, mbali na hayo Dk Mandai inabainisha kuwa pia mbegu za mti wa mlonge hutibu magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweka sawa shinikizo la damu.

Anasema kwamba mbegu za mlonge hali kadhalika zina uwezo wa kutibu baridi yabisi na uvimbe wa magoti , kifua kikuu (TB), kisukari Ukimwi, kukosa usingizi, magonjwa ya zinaa, harufu mbaya mdomoni, vidonda vya tumbo, majipu pamoja na homa ya matumbo.

Magonjwa mengine yanayotibika kwa mbegu hizo ni malaria sugu, pumu, matezi, saratani na maumivu ya mwili huku mafuta ya mbegu hizo yakiwa ni dawa ya kuchua maumivu ya mwili.

Pamoja na hayo, Dk Mandai anaeleza kwamba gome la mlonge linapochemshwa na  kuwa laini ni dawa ya ugonjwa wa bandama, ini, maumivu, tetenasi na kupooza, huku akiongeza kuwa majani ya mlonge yanapopikwa huliwa na kusaidia katika kupambana na uhaba wa vitamin C kwani upungufu wa vitamini hiyo husababisha damu kuvuja kwenye fisi za meno.

Hali kadhalika, majani ya mlonge yanapowekwa kwenye kidonda au uvimbe yanasababisha tiba nzuri, lakini juisi inayotokana na majani ya mlonge ikichanganywa na asali huwa ni dawa nzuri kwa magonjwa ya macho.

Baada ya kuyafahamu hayo yote ni vizuri pia tukafahamu kuhusu mizizi ya mlonge, ambapo Dk Mandai anasema mizizi ya mti mchanga wa mlonge ni tiba nzuri ya mishipa ya fahamu, kifafa, nyongo, baridi yabisi sugu na kujaa maji.

Dk  Mandai ni mtaalam wa tiba asilia mwenye uzoefu katka utoaji wa huduma za tiba  asili, uzoefu ambao ameupata kutoka mataifa ya mengine, ikiwemo Afrika Kusini  na amekuwa akitoa tiba ya magonjwa mbalimbali kwenye kliniki yake ilipo Ukongo Mongolandege jijini Dar es Salaama 


11 comments:

 1. Replies
  1. Kwa hongera kwa utafiti wako wa kina endelea na kazi hiyo ingawa wengi huwapinga kuwa magonjwa Kama Ukimwi hayana dawa huku Mungu anasema ameweka kila maradhi na tiba yake.

   Delete
 2. Replies
  1. Asante sana Japhet Lobulu nawe nashukuru kwa kufuatilia uchambuzi huu

   Delete
 3. Nimejikuta ni mshabiki sana wa uchambuzi wako, Hongera

  ReplyDelete
  Replies
  1. Shukrani sana Mustafa Msenga nitashukuru ukiendelea kuwa karibu nasi kupitia tovuti hii ili kuyafahamu mengi zaidi kuhusu mimea na matunda na faida zake pia

   Delete
 4. Replies
  1. Asante sana Geofrey Bonzo kwa kuwa mfuatiliaji wetu tafadhali endelea kuwa karibu nasi kila siku kupata mengine mengi zaidi kuhusu mimea na matunda na faida zake

   Delete
 5. Asante kwa ufafanuzi huo..mimi na shida na meno vipi naweza pata dawa hapo kwenu?

  ReplyDelete