Tuesday, 20 January 2015

MTOPETOPE NI TUNDA LENYE MAAJABU KATIKA TIBA
Mtopetope ni miongoni mwa maelfu ya aina nyingi za miti asili inayoota katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Katika baadhi ya maeneo mti huu wa matopetope ni maarufu kutokana na matunda yake yanayojulikana kama topetope na si vinginevyo.


Mti huu unaweza kuukuta umeota katika maeneo ya mabondeni au hata milimani, lakini mti huu umekuwa ni muhimu katika kuwapatia matunda watu na inaelezwa kuwa mti huu unamaajabu makubwa katika kutibu maradhi mbalimbali.

Kwa mujibu wa mtaalam wa tiba asili, kutoka Mandai Herbalist Clinic , Dk Mandai anasema mti huo una maajabu makubwa katika tiba ambapo inaonesha kuwa mti huo ulitumiwa na wazee katika kutibu magonjwa mbalimbali kipindi cha miaka mingi iliyopita.

Miongoni mwa magonjwa ambayo mti huo unaweza kuyatibu hata sasa ni pamoja na ya wanawake hasa ya sehemu za siri.

Dk Mandai anasema wanawake wanaotoa maji yenye mwasho na mengine kama maziwa sehemu za siri wanaweza kutibiwa na mti huu na kupona kabisa.

Dokta anaendelea kufafanunua kwamba mara nyingi wanawake kutokana na maumbile yao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya magonjwa hayo ambapo miongoni mwa athari kubwa ni kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

Aidha, anasema kwamba mti huo pia unaweza kurudisha sehemu za siri za mwanamke zilizoharibika  hususani wakati wa uzazi.

“Mwanamke ambaye ameharibika sehemu zake za siri kutokana na uzazi mti huu ni tiba nzuri sana ambapo unatakiwa kuchemsha majanai na kisha aoshe sehemu husika,” alisema Dk Mandai.

Mbali na hayo, mti huo pia unasaidia kutibu maradhi ya vidonda vya tumbo na magonjwa ya moyo ambayo yanawakabili watu wengi hasa katika kizazi cha sasa.
Sambamba na  hayo Dk Mandai anasema magome ya mtopetope husaidia kutibu vidonda.

“Kila mwenye uvimbe au kidonda achukue gome la mti huu aliponde kisha abandike eneo husika na kidonda hicho kitapona,” alisema Dk Mandai.

Dk Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam anasema endapo utakuwa unatatizo la kiafya usikate tamaa na badala yake unaweza kufika kituoni Mongolandege na kupatiwa matibabu sahihi kutokana na tatizo lako amini kwamba magonjwa mengi yanatibiwa kwa dawa asili.

No comments:

Post a Comment