Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 31 January 2015

MWAROBAINI NI SULUHISHO LA MAGONJWA MENGI
Mwarobaini ni mti maarufu sana na unajulikana karibu kila mahali , huku ukielezwa kuwa mti huo ni kati  ya miti mirefu yenye ukijani mzuri sana, ingawaje majani yake ni machungu mno.

Mti huo umekuwa ukifahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali, huku ikiaminika kwamba  mti huo asili yake ni nchini India. Pia mwarobaini hustawi zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili hali ya ukame.  


Kwa hapa nchini, mti wa mwarobaini huweza kupatikana kwa urahisi kabisa katika maeneo mengi ya mijini na vijijini pia.

Jina la mti huu ‘mwarobaini’ linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini, huku majani yake na mbegu zikitumiwa kama tiba kwa miaka.

Mtaalam wa tiba asili hapa jijini Dar es Salaam Dk Abdallah Mandai, anasema kwamba magome ya mti wa mwarobaini yakichemshwa huwa ni dawa ya kuua minyoo yote tumboni, homa, kikohozi na kujisikia kuwaka moto, kuharisha pamoja na tatizo la vidonda vya tumbo, n.k

Aidha, mtaalam huyo anasema kuwa majani ya mti huo yanapowekwa katika maji moto huweza kutibu matatizo ya macho, maumivu ya ini pamoja na magonjwa ya ngozi.

Pamoja na hayo, Dk Mandai anabainisha kuwa matunda ya mti wa mwarobaini pia yanaelezwa kusaidia matatizo ya matezi, bawasira pamoja na matatizo ya meno, huku akiongeza kuwa mti huo pia umekuwa ukisaidia katika kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi.

Msomaji wetu wa tovuti hii tunapenda kukuhamasisha kuendelea kupenda kutumia mimea asili kama tiba muhimu kwa afya yako, lakini pia unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utakutana na mtaalam wa tiba hizi asili Dk Abdallah Mandai na hakika utapata suluhu la matatizo yako ya kiafya.

No comments:

Post a Comment