Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 28 January 2015

NANASI TUNDA LENYE UWEZO WA KULINDA AFYA ZETU

Nanasi ni tunda lenye vitamin nyingi pamoja na madini ya chuma, copper na phosphorous, huku miongoni mwa vitamin hizo zikiwa ni pamoja na vitamin A, B, C, lakini pia tunda hili husaidia kutengeneza damu na kuimarisha mifupa, meno neva na misuli (muscles).


Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai, kutoka Mandai Herbalist Clinic anaeleza kwamba mizizi ya mmea wa nanasi inapochemshwa huweza kutumika kama dawa ya matatizo ya figo na kuua minyii mwilini.

Aidha, mtaalam huyo anaendelea kusema kwamba utomvu wa tunda hili pia ni dawa ya chunjua pamoja na magonjwa ya koo, huku juisi ya majani ya tunda hili yakielezwa kuwa ni dawa ya vidonda na shida za ngozi na majipu.

Pia Dk Mandai anaongoza kwamba, maua ya mmea wa nanasi yanapoongezwa na asali huwa inakuwa ni tiba ya mafua na kikiohozi, ambapo mgonjwa atapaswa kutumia kijiko kidogo kila anapotumia dawa hiyo.

Mbali na hayo, mtaalam huyo anasbainisha magonjwa mengine ambayo huweza kutibiwa na nanasi kuwa ni pamoja na matatizo mbalimbali ya tumbo, magonjwa ya bandama (spleen), ini na utumbo mwembamba, pumu, kurudisha kumbukumbu pamoja na homa.

Hali kadhalika, tunda hili huwasaidi kina mama juu ya changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuthibiti matatizo fulani ya kike, ambayo husababishwa na upungufu wa shughuli za ‘hormones’ au makosa fulani katika sehemu ya yai.

Hata hivyo, Dk Mandai anasema kuwa nanasi pia husaidia kuondoa tatizo la shida ya kufunga choo, baridi yabisi pamoja na kuwa msaada mkubwa kwa kinamama wanaonyonyesha walio na maziwa machache na hata walio na ujauzito wanashauriwa kutumia sana tunda hili kwani pia ni msaada katika kuondoa gesi tumboni.

Mtaalam huyo wa tiba asili anabainisha kwamba ni vizuri kutumia glasi moja hadi mbili kwa siku ya juis ya tunda hilo, lakini ni vyema kufika kituoni Mandai Herbalist Clinic endapo utakuwa unasumbuliwa na maradhi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment