Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 28 January 2015

MCHAI CHAI NI TIBA KWAKO
Mchai chai ni mmea ambao unatambulika hapa nchini pamoja na Afrika kwa ujumla wake, lakini hapa nchini wengi huutambua mmea huu kama kiungo katika chai na husaidia kinywaji hicho kuwa na harufu mwanana zaidi na kuwavutia watumiaji.
Mtaalam wa tiba asili hapa nchini Dk Abdallah Mandai yeye anabainisha kuwa mmea huu una faida nyingi na ni dawa kwa matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzuia kutapika, kutuliza tumbo endapo linauma, kuharisha sambamba na kutibu homa.

Pia mtaalam huyo anaeleza kuwa, mmea huo husaidia kukabiliana na tatizo la baridi yabisi, kusafisha figo, kuwasaidia wale wenye shida ya matumbo kuunguruma na hivyo kumsaidia mhusika kurejea katika hali ya kawaida.

Hali kadhalika, Dk Mandai anasema kuwa “unapotumia mchai mchai husaidia uyeyushaji wa chakula na magonjwa ya damu pamoja na matatizo ya athma  na kuondoa maumivu ya mbalimbali mwilini.

Mchai chai pia husaidia kuwaondolea maumivu kinamama wakati wa hedhi na husaidia kutibu matatizo ya ukosefu wa usingizi  pamoja na magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya sufuria za aluminiaum na shinikizo la damu.

Dk Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam anasema mchai chai huo unaweza kutumika kwa kuweka majani yake kwenye maji yaliyochemshwa, kwa dakika kumi na tano, kisha mhusika atatakiwa kunywa nusu ya kikombe kutwa mara tatu

No comments:

Post a Comment