Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Saturday, 24 January 2015

NYANYACHUNGU NI MBOGA YENYE UWEZO WA KUKUKINGA NA MARADHINi wazi kwamba watu wengi wamekuwa wakitumia nyanyachungu au kwa jina jingine (ngongwe) kama mboga, lakini wengine hutumia nyanyachungu katika kuhakikisha wanaongeza radha katika chakula.

Nyanyachungu huzalishwa kutokana na mmea ambao hukua kufikia urefu wa mita moja hadi moja na nusu, matawi na majani yake hufanya kichaka.

Nyanyachungu zinaweza kuwekwa katika makundi mawili zinazotoa matunda madogo madogo na nyingine matanda makubwa na machungu kiasi. Sina uhakika ni kwanini zinaitwa jina hilo, lakini huenda ni kutokana na kuwa na ladha ya uchungu kiasi.

Rangi ya matunda ya nyanyachungu huweza kuwa ya kijani kibichi au njano na nyeupe wakati yanapokuwa yakipevuka kabisa hugeuka na kuwa na rangi nyekundu.

Nyanyachungu zinapopevuka kabisa huwa hazifai kuliwa tena , na wengi huzitumia katika kujipatia mbegu kwa ajili ya kupanda, lakini pia mmea wa nyanyachungu unauwezo mkubwa wa kustahimili upungufu wa maji kuliko aina nyingine za mboga.

Wakati wengi wakizitumia nyanyachungu kama mboga, Tabibu wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema nyanyachungu ni dawa nzuri kwa wanaosumbuliwa na maradhi ya tumbo.

Anasema kwenye nyanyachungu kuna kiwango kikubwa cha madini, lakini pia kuna kiwango kikubwa cha madini pamoja na vitamin A, B na C.

Dk Mandai, anabainisha kwamba kutokana na wingi wa vitamin na madini nyanyachungu  inatibu maradhi mengi yakiwemo ya matumbo.

Dk Mandai anasema kuwa wakazi wa maeneo ya baridi na Pwani mara nyingi husumbuliwa na maradhi ya tumbo na hivyo ni vyema wakaitumia nyanyachungu ili kuepukana na maradhi   hayo.

“Ndani ya nyanyachungu mna tiba au ni maajabu makubwa katika tiba. Mna vitamin A,B na C. lakini pia mna kiwango kikubwa cha madini” anasema Dk Mandai.

Pamoja na hayo, Dk Mandai anabainisha kuwa kwa wanaume wanaosumbuliwa zaidi na tatizo la ngili sanjari na tatizo la kujaa gesi na kutopata choo vizuri. Anasema mtu anaweza kujisikia tumbo limejaa isivyo kawaida hata kama hajala chochote, lakini hali hiyo inaweza kupatiwa ufumbuzi kutokana na matumizi stahiki ya nyanyachungu.

Hali kadhalika, mtaalam huyo anasema kwamba nyanyachungu zinasaidia kupambana na magonjwa mbalimbali, na hivyo ni vizuri kutumia chakula kuwa tiba badala ya dawa kuwa tiba.

Hizo ni baadhi ya faida unazoweza kuzipata kupitia nyanyachungu, ama hakika tumejaliwa kupata mimea tiba ambayo ndani yake ni tiba na iwapo unasumbuliwa na maradhi yoyote ni nafasi yako sasa kufika Mandai Herbalist Clinic kwa lengo la kupata matibabu bora yenye kutumia dawa asili zitokanazo na mimea na matunda.


No comments:

Post a Comment