Tunda hili linapotengenezwa kama kinywaji (juis)
husaidia kuondoa maumivu ya tumbo na kuponya vidonda vya tumbo pamoja na kurekebisha
udhaifu mwingine tumboni.
Dk Abdallaah Mandai anaeleza kuwa tunda hilo
husaidia kuongeza nguvu za mwili na ubongo sambamba na kujenga neva na fahamu.
Aidha, mtaalam huyo anabainisha kwamba, tunda hilo
pia huweza kumpatia mtu uwezo mzuri wa kuona, huku majani yake yakielezwa
kuongeza damu na kusheheni vitamin A, B, C na E.
Dk Mandai anasema kuwa, vyakula kama nyama husababisha
'uric acid' nyingi mwilini, ambayo husababisha magonjwa mengi mwilini, hivyo
tunda hili huweza kusafisha hiyo na kuitoa nje na kuondoa magonjwa pia.
“Tunda
hili hufanya vizuri sana kwa magonjwa hayo na kuyamaliza, lakini pia
husaidia wanawake katika kuifanya hedhi iende vizuri kila mwezi,”
alisema mtaalam huyo.
Pia majani yake yanapochemshwa kama chai na mtu
kunywa husaidia kuondoa matatizo mwilini, ikiwa ni pamoja na uchovu, udhaifu na kujisikia ovyo,
kuumwa kichwa, koo (throat), tumbo, mapafu na uvimbe.
Hali kadhalika, unapotafuna majani yake husaidia
kutibu vidonda vya mdomo (ufizi) na kuimarisha meno pamoja na kuondoa maumivu.
Pamoja na hayo, Dk Mandai anasema parachichi huweza
kutumika hata katika masuala ya urembo, ambayo ni pamoja na kukuza nywele na
kuokoa wale wenye tatizo la nywele zinazoanguka.
Hayo ni machache tu kuhusu parachichi, hivyo ni
vizuri ukaendelea kutembelea tovuti (website) hii mara kwa mara kwa ajili ya kufahamu mambo
mengi juu ya tiba asili na halisi za mimea na matunda, lakini pia tunakaribisha
matangazo ya biashara ambapo unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0672 060 006
/ 0758 163 818 na uanze sasa kutangaza nasi. Karibu!!
No comments:
Post a Comment