Tuesday, 27 January 2015

SOYA NI NZURI KWA AFYA ZETU KAMA ITATUMIKA IPASAVYOSoya ni mmea ambao huwekwa katika kundi la jamii ya maharage na ni chakula ambacho huliwa na watu wa mataifa mbalimbali duniani, lakini mbali ya kuwa chakula pia ni dawa.


Soya ni moja ya chakula chenye vitamin ya kutosha mwilini ikiwa ni pamoja na vitamin A, B Complex, C, D. E, F, G, H, na K na kutokana na uwingi wa vitamin hizo soya imekuwa ni sehemu muhimu ya chakula kwa muda mrefu, hata kupelekea jamii ya watu wa china kufanya kuwa ni moja ya chakula cha heshima kwao.

Mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbalist Clinic Dk Abdallah Mandai, anasema kwamba soya ni moja ya chakula hapa duniani chenye vitamin nyingi zaidi, lakini pia huwa na mafuta ambayo husaidia chakula kuwa kitamu.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa kutokana na ubora wa soya ilipelekea watu wa zamani kukitumia chakula hiki kama mbadala wa nyama, mayai na mafuta (butter)  hii ilimaanisha walipokosa hivyo walikuwa wakitumia soya.

Mtaalam huyo wa tiba asili anasema watu wa Asia hutumia maziwa ya soya kuwalisha watoto na wazee, moja ya sababu ikiwa ni kutokana na uwezo wake wa kuwasaidia watoto wenye tatizo la utapia mlo.

Mbali na hayo, pia soya inayo ‘glycelin’  pamoja na ‘faty acid’ ambayo husaidia ufanyaji kazi wa ubongo na maini, huku ikielezwa kuwa ni chakula  kizuri kwa ajili ya mishipa ya fahamu iliyochoka kutokana na kuwa na ‘licithin’  hivyo kuifanya soya kuendelea kuwa chakula kizuri sana kwa wazee au watu wadhaifu na watoto.

Aidha Dk Mandai anaendelea kusema kuwa, unga wa soya una utajiri mwingi wa protini, kuliko unga wowote utokanao na jamii ya mikunde (legumes) kama njegere,  maharage ya kawaida na mikunde, hali kadhalika unga huo wa soya pia una wanga chini ya asilimia mbili, wakati jamii nyingine huwa na wanga wa karibu mara 30.

Pia soya ina kiwango cha ‘calcium’  mara 20 ya zaidi ya viazi na mara 12 ya ‘calcium’ inayopatikana kwenye unga wa ngano pamoja na mara 5 zaidi yake ya mayai na mara 2 ya ile ya maziwa ya maji.

Hali kadhalika mtaalam huyo anabainishwa kwamba, kilogramu moja ya unga wa soya ni sawa na protini katika mayai sabini (70) na kilogramu moja ya unga huo wa soya pia ni sawa na protini katika nyama kilo tatu (3), lakini pia kilogramu hiyo hiyo moja ya unga wa soya ni sawa na protini inayopatikana katika maziwa lita 112 .

Sambamba na hayo, Dk Mandai anafafanua kuwa soya inauweza kutibu tatizo la vidonda vya tumbo, saratani (cancer) na husaidia kumpatia nafuu mgonjwa wa kisukari na wale wenye kusumbuliwa na matatizo ya kibofu pamoja na figo.

Lakini pia mafuta ya soya yanapotumika kwa kupakwa kichwani huondoa mba na ukurutu, huku mbegu zake zinapolowekwa na kisha zikavimba na kupondwa husaidia ukuaji wa nywele na hata kwa wale wenye kipara huota.

Hizo ndizo baadhi ya faida za soya kiafya endapo ungependa kufahamu undani wa haya zaidi ni vyema ukafika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment