Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 23 January 2015

TANGO NI TUNDA LENYE MSAADA KATIKA MAISHA YETU
Mara  nyingi tumekuwa tukisikia kwamba mboga za majani na matunda ni kinga kwa afya yako na ni wazi na ukweli kwamba matunda mengi yana manufaa kwa afya na miongoni mwa matunda hayo ni pamoja na tango.


Hapa Mandai Herbalist Clinic inakufahamisha baadhi ya faida za tango kiafya.
Pamoja na kuwa na kukosa ladha ya utamu, lakini ni vizuri ikafahamika tunda hili linasifa kwa kuwa na vitamin zote unazohitaji kwa siku. Tango moja lina vitamin B1, B2, B3, B4, na B6 madini ya chuma, 'potassium' na 'zinc.'

Pili unapojisikia kuchoka mchana, unaweza kula tango moja ambalo linaweza nguvu kwa saa kadhaa.

Tatu, ngozi yako inahitaji tango  kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Weka au sugulia vipande vya tango usoni  au sehemu iliyoathirika na utaona maajabu baada ya siku chache.

Lakini pia inaelezwa kuwa tango huweza kusaidia tatizo la midomo kukauka, katika hili inatakiwa kuchukuwa kipande cha tango na sugulia mdomoni kwa taratibu bila kutumia nguvu, hii itakusaidia baada ya siku kadhaa kuondokana na tatizo hilo.

Hali kadhalika inaelezwa kuwa tango linaweza kukupa msaada katika shughuli za usafi, hii ni kwa sababu unaweza kuchukua kipande cha tango na kusugulia viatu vyako, inaelezwa kuwa husaidia kung'aza viatu, lakini mbali na hilo pia inaaminika tunda hili huweza kusaidia kusafishia vioo ambavyo vimefubaa kwa uchafu au maji ya chumvi.

Asante kwa kuendelea kutembelea tovuti hii tambua kuwa tunathamini sana uwepo wako wewe msomaji wetu na mfuatiliaji wa tovuti hii na itapendeza endapo ukiamua kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kuhusu kutembelea tovuti hii na kupata faida juu ya mambo mbalimbali kuhusu afya pamoja na tiba asilia.


No comments:

Post a Comment