Tuesday, 27 January 2015

TENDE ZINAELEZWA KUWA NA FAIDA LUKUKI KWA AFYA
Tukizungumzia matunda ambayo yamekuwa yakiaminika kuwa ni tiba basi hatuwezi kuacha kulitaja hili tunda linalofahamika kama tende, ambalo linaaminika kuwa msaada mkubwa kwa binadamu endapo litatumika ipasavyo.


Tunda hili ni maarufu katika nchi za Mashariki ya Kati na sehemu nyingine duniani. Asili kamili ya tunda hili ni kutoka katika nchi za Kiarabu na liliingia Afrika Mashariki mnamo karne ya 7.

Hapa nchini Tanzania, tende hupatikana kwa wingi kisiwani Zanzibar pamoja na Pemba, ambapo imekuwa kama ni sehemu ya chakula cha kiutamaduni visiwani humo.
Mbali na ladha yake kuwa nzuri na yenye kuvutia , na kuwafanya watu wengi kulipenda tunda hili, lakini pia tunda hili limekuwa likitajwa katika vitabu vitukufu vya dini.

Aidha, tunda hili limekuwa likitumiwa sana na waumini wa dini ya Kiislamu hususani katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na uwezo wake wa kurejesha nguvu mwilini kwa haraka zaidi.

Mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbalist Clinic, Dk Abdallah Mandai anasema kuwa tende ni chanzo kizuri cha virutubisho na nishati mwilini, lakini pia huuwezesha mwili kujipatia nguvu kwa haraka sana na hiyo ndio sababu ya tunda hili kutumika kwa wingi katika Mfungo wa Ramadhani, kwani waumini waliofunga hulitumia tunda hili ili kurudisha nguvu na nishati iliyopotea mchana kutwa walipokuwa wamefunga.

Aidha, Dk Mandai anaeleza kuwa ndani ya tende kuna virutubisho kama vile ‘calcium,’ protein,’‘potassium,’‘magnesium,’phosphorous,’vitamin A’foliate’ na‘carbohydrates,’ ambazo zote kwa pamoja ni muhimu katika miili yetu kiafya.
Hata hivyo, mtaalam huyo anafafanua kuwa tende ni chakula cha afya na huwa na mkusanyikowa ‘vitamin A,’ ambayo husaidia katika kuongeza nuru ya macho. Pia, ndani yake kuna madini ya ‘calcium,’ ambayo husaidia kuimarisha mifupa, hali kadhalika ndani ya tunda kuna‘vitamin B6’ na B12, ambazo husaidia katika usagaji na ufyonzaji mzuri wa chakula na kuingia katika mishipa ya damu.

Mbali na hayo, tende pia hutibu maradhi ya tumbo kama vile kujaa gesi, kuharisha na kuchafuka kwa tumbo, huku akibainisha kuwa pia tende husaidia kuondoa sumu mwilini na kusaidia kuongeza nguvu za kiume endapo litatumika kwa kufuata ushauri wa kitabibu.

Pamoja na hayo, tende ni tunda la pekee lenye uwezo wa kuupa mwili vitu vine kwa wakati mmoja ambavyo ni protini, wanga,vitamin na mafuta. Pia ni tunda ambalo huyeyuka haraka sana tumboni, hivyo kutolipatia tumbo shida ya kufanya umeng’enyaji (digestion).

Pia anaeleza kuwa tende ni chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kutokana na kusaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu ambavyo humfanya mtoto kuwa na afya bora.

Zaidi ya yote hayo, uwepo wa madini ya chuma ndani ya tende, husaidia kuwapa ahueni watu wenye upungufu wa damu mwilini. Hivyo basi, mbali nakupenda kutumia tende kipindi cha Mwezi wa Ramadhani tu, ni vizuri tukatumia siku zote kama jinsi tunavyotumia vyakula vingine, ili kuweza kuimarisha afya zetu kikamilifu.Mandai Herbalist Clinic inakuarifu kuwa endapo unasumbuliwa na maradhi yoyote ni vyema ukafika Ukonga, Mongolandege mahali ilipo kliniki hii kwa ajili ya kupata suluhisho la matatizo hayo kwa kutumia dawa asili zitokanazo na mimea na matunda na zisizo na kemikali.

No comments:

Post a Comment