Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 29 January 2015

TIKITI MAJI LINAWEZA KUWA MKOMBOZI WA AFYA YAKOTikiti maji ni kati ya matunda yenye maji mengi na matamu  ndani yake na pia tunda hili lipo katika jamii ya maboga. Tunda hili linafaida kadhaa katika masuala ya afya hususani pale linapotumika ipasavyo.
Mtaalam wa tiba asili hapa nchini Dk Abdallah Mandai, anasema miongoni mwa faida zinazotokana na kutumia tunda hili ni pamoja  na kusaidia kuondoa matatizo ya maumivu ya viungo, tumbo, baridi yabisi na matatizo ya figo nk.

Watu wengine ambao huweza kupata ahueni kwa kutumia tunda hili ni pamoja na wale wenye matatizo ya kifua na mapafu, kuzidiwa na protini mwilini, wenye shida ya usagaji wa chakula pamoja na wale wanohitaji kupunguza unene basi ulaji wa tunda hili huweza kusaidia sana.

Dk Mandai anabainisha kwamba, mbegu zake zinapoliwa husaidia kushusha shinikizo la damu na zikikaangwa na kusagwa huwa ni dawa ya maumivu wakati wa kujisaidia, lakini pia zinasaidia kuondoa  maumivu ya tezi la mamalia la mbegu za kiume. 

Mbali na hayo, mtaalam huyo anafafanua kuwa maji yake (juisi) ya tunda hili lililoiva ni dawa ya kuyeyusha mawe katika figo na kibofu. Pia ganda la tunda hilo linapopondwa huwa ni tiba ya kubandika juu ya ngozi yenye shida.

Pamoja na hayo, Dk Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anaongeza kwamba mbegu za tikiti maji zikikaangwa na kisha kusagwa na mgonjwa akanywa huweza kutibu kifua kikuu  kwa mhusika endapo mhusika  atakuwa akitumia vijiko viwili kutwa mara mbili.
Mandai Herbalist Clinic ni kituo cha tiba mbadala kinachopatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam, hivyo unaweza kufika katika kituo hiki na utapata ufumbuzi wa matatizo ya kiafya.

No comments:

Post a Comment