Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 30 January 2015

TUNDA LA KOMAMANGA NI DAWA ENDAPO LIKITUMIKA VIZURI
Komamanga ni moja ya tunda lenye ladha nzuri sana na hupatikana sana katika maeneo ya Afrika Mashariki, lakini pia ni dawa nzuri kwa magonjwa mengi.

Mtaalam wa tiba asili hapa nchini Dk Abdallah Mandai anasema kuwa, miongoni mwa magonjwa yanayoweza kupata suluhu kutokana na mmea huu ni pamoja na magonjwa kuharisha damu, ambapo mgonjwa atapaswa kutumia juisi ya majani mabichi na machanga pia.

Aidha, anaendelea kusema kwamba maganda ya tunda hilo pia ni dawa nzuri ya kwa wale wenye matatizo ya kuhara, huku majani yake pia yakielezwa kuwa ni dawa nzuri ya virusi vya macho (conjuctivity virus).

Pia komamanga linasaidia kutibu ugonjwa wa malaria, vidonda vya kuoo sambamba na homa zote, hii ni pale ambapo magome yake yatachemshwa kisha mgonjwa anywe maji yake.

Komamanga likiwa katika mti wake
Mtaalam huyo anafafanua kuwa komamanga husaidia kwa kutibu wale wenye matatizo ya pumu, matatizo ya njia ya mkojo, kuweka sawa mfumo wa chakula pamoja na kutibu ini na njia ya usagaji wa chakula.

Tabibu huyo anasema gramu 10 hadi 15 katika lita ya maji na iwe iwe ni majani, magome au maua.


Hayo ni machache tu kuhusu komamanga, hivyo ni vizuri ukaendelea kutembelea tovuti (website) hii mara kwa mara kwa ajili ya kufahamu mambo mengi juu ya tiba asili na halisi za mimea na matunda, lakini pia tunakaribisha matangazo ya biashara ambapo unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0672 060 006 / 0758 163 818 na uanze sasa kutangaza nasi. Karibu!! 


No comments:

Post a Comment