Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 31 January 2015

UGONJWA WA EBOLA WAENDELEA KUSABABISHA VIKWAZO KATIKA SEKTA YA ELIMU


Kufuatia kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola nchini Liberia, imeilazimu nchi hiyo kuhairisha kufunguliwa kwa shule zote nchini humo kutokana na sababu ya kutojiandaa kikamilifu katika kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.
Nchini Liberia shule zilifungwa mnamo mwezi Julai mwaka jana, ikiwa ni miongoni mwa jitihada za kukabiliana na janga hilo na serikali ya nchi hiyo ilikuwa imepanga kuanza kufunguliwa kwa shule hizo kuanzia siku za Jumatatu.

Aidha, miongoni mwa sababu zilizoelezwa kupelekea kushindwa kufunguliwa kwa shule hizo ni pamoja na ukosefu wa maji ya kuoshea mikono pamoja na ukosefu wa vifaa vya kupima joto la mwili.

Hata hivyo, kwa sasa nchi hiyo ina jumla ya visa vitano tu vilivyothibitishwa na inaelezwa kwamba ugonjwa huo tayari umesababisha vifo vya watu wapatao 3600 kwa nchini humo Liberia.

No comments:

Post a Comment