Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 20 January 2015

UKOSEFU WA NGUVU ZA KIKE NI TATIZO AMBALO LIPO LAKINI HALIPO WAZINi nadra sana kusikia watu wakizungumzia matatizo ya nguvu za kike, badala yake tumekuwa tukisikia matatizo sana kuhusu matatizo ya nguvu za kiume.

Matatizo ya nguvu za kiume si tu yanazungumzwa na watu wa makundi mbalimbali, lakini pia hata waganga wengi wa tiba asili na mbadala wamekuwa wakishuhudiwa wakitundika  mabango yao yenye kujinadi kuwa wanatibu matatizo hayo ya nguvu za kiume.


Ni dhahiri kuwa hakuna mabango yanayoonesha kutibu nguzi za kike na kama yapo basi ni machache hivyo kuifanya jamii ione kuwa tatizo hilo halipo kwa wanawake licha ya kwamba tunajua kuna ugumba na utasa.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai kutoka akituo cha Mandai Herbalist Clinic kilichopo Mongolandege jijini Dar es Salaam anasema wanawake wengi wanasumbuliwa na matatizo ya nguvu za kike.

Dk Mandai anasema kutokana na tatizo hilo kuwa wazi zaidi kwa wanaume kwa maana ya maumbile yao, ni rahisi kujulikana huku wanawake wengi wakikabiliwa nalo lakini halijulikani.

Aidha, tabibu huyo anabainisha kuwa tatizo hilo halijulikani kwa sababu si rahisi kumgundua mwanamke mwenye tatizo hilo nah ii ni kwa sababu wanawake wengi wenye tatizo hili hujifanya kama hawana shida hii na pale wanapokuwa na mwanaume huonesha kwamba anazo hisia ya kutaka kufanya tendo la ndoa huku uhalisia ukiwa hajisikii chochote.

Dk Mandai anasema kuwa tatizo hilo husababishwa na homoni za mwanamke kutokuwa za kawaida ama kuwa za juu zaidi ama chini.

“Kwa kawaida homoni za mwanamke inabidi ziwe 3269 au 8840 zikiwa chini ya hapo ama juu mwanamke huyo anakuwa na tatizo la kutojisikia hamu ya kushiriki tendo la ndoa, lakini anapokuwa na mwanaume anaweza kujionesha kama yupo tayari kwa tendo hilo huku uhalisia ukiwa ni hapana,” alisema Dk Mandai

Aidha, Dk Mandai anaendelea kusema kwamba kuwepo kwa kiwango cha chini cha homoni kunamfanya mwanamke akose hisia za kufanya tendo hilo licha ya kwamba anaweza kuonekana kama hana tatizo hilo.

Dk Mandai anasema kuwa licha ya ukubwa wa tatizo hilo lakini wengi wao hukosa ujasiri wa kwenda kwa matabibu wa tiba asili au madaktari kuwaeleza ili wapatiwe suluhisho kwa sababu linatibika.

Ni vigumu wanawake kueleza matatizo yao ya kutojisikia hamu ya tendo la ndoa,” alisema Dk Mandai.
 
Mbali na hayo, Daktari anasema mwanamke mwenye tatizo hilo anashauriwa kutumia mboga za majani kwa wingi pia ale tende, halua na asali, lakini pia Dk Mandai  anasema kwamba kupitia Mandai Herbalist Clinic anatoa dawa ambazo huamsha homoni na hivyo kumfanya mwanamke kusika kuondokana na tatizo hilo na hivyo kufurahia tendo la ndoa.

No comments:

Post a Comment