Tuesday, 20 January 2015

UKWAJU UNAWEZA KUWA HITIMISHO LA MATATIZO YA AFYA YAKO
Ukwaju ni tunda linalotokana na mkwaju, mkwaju ni mti unaotoa matunda ambayo yanajulikana kama ukwaju ambayo wengi huyatumia kwa kula au kutengenezea juisi.

Bila shaka kumekuwepo na watu wengi ambao hutumia tunda hili lenye ladha ya ugwadu (uchachu) kwa kutengenezea hasa juisi ambayo hutumika kama kinywaji kinachoburudisha. 

Lakini matabibu wamekuwa wakieleza kwamba mti wa mkwaju unafaida nyingi kwa binadamu tofauti na wengi wanavyodhani.

Mtaalam wa tiba asili, Dk Abdallah Mandai anasema mti huo unafaida kuanzia mizizi, magome, majani, na hata matunda yake pia,  huku akibainisha kuwa mti huo unategemewa katika tiba za magonjwa mbalimbali yanayowakabili wanadamu wengi hususani katika kizazi hiki cha sasa.

Dk Mandai anasema “tukianza mizizi ya mkwaju ikitengenezwa vizuri huwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengi likiwemo tatizo la mkojo mchafu (UTI)”

Pia Dk Mandai anabainisha kuwa mizizi inasaidia sana kuzibua mirija ya uzazi, lakini pia humpunguzia mwanamke maumivu wakati wa hedha au wakati wa tendo la ndoa.

Aidha, anafafanua kuwa majani ya mkwaju yanapoandaliwa vizuri husaidia sana kuzuia homa za mara kwa mara ukiwemo ugonjwa wa malaria, kuharisha damu, homa ya matumbo pamoja na vidonda vya tumbo.

Hali kadhalika, Dk Mandai anasema majani ya mkwaju yanapokaushwa kivulini kasha kupondwa na unga wake ukichanganywa na mafuta ya nazi husaidia kuondoa magonjwa ya ngozi na mwasho.

“Kwa wenye matatizo ya miguu kwa kufa ganzi au kuwaka moto wachanganye unga wa majani ya ukwaju na mafuta ya nazi kisha mgonjwa achue eneo husika maumivu yanaondoka kabisa,” alisema Dk Mandai.

Mbali na faida hizo, lakini pia unga huo  wa majani ya ukwaju husaidia sana kwa wale wenye matatizo ya pumu (athama), ambapo mgonjwa anapaswa kuchanganya unga huo pamoja na asali kisha mgonjwa anatakiwa alambe  husaidia sana kuondokana na hali hiyo pamoja na kifua kikavu.

Sambamba na hayo, Dk Mandai anasema kwamba  “ nashauri kuwa mtu atumia juisi ya ukwaju daima anagalau anywe mara mbili au hata tatu kwa siku . Kwanza inaongeza  vitamin A, B na C, lakini pia ina madini ya chuma, ‘calcium’ na ‘zink’.

Pia kwa wale wenye shida ya kupata choo au tumbo kuunguruma ni vizuri wakatumia juisi hiyo itawasaidia kuondokana na matatizo hayo.

Hizo ni baadhi tu ya faida chache za mkwaju, hivyo kutokana na hayo machache Dk Mandai anapenda kutoa wito kwa Watanzania kutokata miti hovyo na badala yake tuongeze juhudi katika kupanda miti zaidi kwani  miti imekuwa na faida nyingi sana na hasa pale inapotumika kama dawa na kutusaidia kurekebisha afya zetu pale zinapoteteleka.

Unaweza kukutana na Dk Mandai kwa kufika kituoni Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam ambacho kinafahamika kwa jina la Mandai Herbalist Clinic na utakutana na huduma nzuri na salama kwa afya yako .

No comments:

Post a Comment