Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 29 January 2015

VIRUSI VYA EBOLA VYAELEZWA KUANZA KUWA SUGU
Wanasayansi wanaokabiliana na janga la Ebola nchini Guinea wanasema kwamba virusi vinavyosababisha ugonjwa huo vimeanza kujibadilisha umbo na kuwa sugu hali inayopelekea ugumu kutibu ugonjwa huo. 

Kauli ya wanasayansi hao inasikika kwa mara ya kwanza tangu ugonjwa huo kugunduliwa mnamo mwezi Machi mwaka jana.

Aidha, taarifa zinasema kwamba watafiti katika taasisi ya Pasteur mjini Paris Ufaransa, wamekuwa wakichunguza mamia za sampuli za damu ili kujaribu kubuni mbinu za kupambana na virusi hivyo. 

Hata hivyo, wanasayansi hao kwa sasa wanajaribu kubaini ikiwa kujibadili kwa umbo la virusi hivyo, kutasababisha maambukizi zaidi na ikiwa wanaweza kufanya lolote kuhusu ambavyo ugonjwa huo unapimwa mwilini na pia ambavyo madawa yanatumika mwilini kupambana na ugonjwa huo.

Mbali na hayo, pia wanasayansi wanataka kuchunguza na kufanyia utafiiti chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Ugonjwa huo wa Ebola umewaua watu zaidi ya elfu nane huko magharibi mwa Afrika, huku  wengi wakiwa ni kutoka Guinea, Sierra Leone na Liberia.

No comments:

Post a Comment