Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 30 January 2015

ZABIBU NI MATUNDA YANAYOWEZA KUKUOKOA DHIDI YA MARADHI YA MOYO
Zabibu hujulikana kama chanzo kizuri cha divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda na tunda hili hukuwa katika kichana chenye zabibu 6 hadi 300.


Matunda haya inaelezwa kwamba yalianza kulimwa huko nchini Uturuki, lakini kwa hapa kwetu nchini yanapatikana sana mkoani Dodoma.

Matunda haya huwa na rangi ya nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza , njano, kijani na hata pinki, licha ya kwamba hapa kwetu Tanzania wengi tumezoea hayo ya rangi inayoonekana (pichani hapo juu)

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula  na Kilimo Duniani (FAO) linaeleza kuwa asilimia 71 ya zabibu yote duniani hutumika kutengenezea  mvinyo na asilimia 27 huliwa kama matunda ya kawaida, huku asilimia 2 ikifanywa kukaushwa.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema kwamba zabibu husaidia kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.

Aidha, anaeleza kwamba zabibu pia husaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia isigande  ndani ya mishipa ya damu, hivyo kutokana  na sababu hii hupunguza hatari ya kukubwa na kiharusi (stroke)

Anaendelea kueleza kwamba zabibu pia inasaidia kuzuia na kutibu tatizo la upungufu wa damu na kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili pia.

Hali kadhalika, Dk Mandai anbainisha kuwa matunda hayo husaidia katika tiba na kinga ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Dk, Mandai anaongeza kwa kusema kwamba zabibu pia husaidia kuimarisha afya ya figo na kuifanya kuwa na uwezo zaidi katika katika kuondosha sumu ndani ya damu .
Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari yake ya asili hivyo huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja.


Sambamba na hayo, mtaalam huyo anaeleza kuwa juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa haja kubwa , lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng;enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.

Divai pia husaidia bacteria rafiki kwa binadamu wanaoishi ndani ya tumbo (normal flora) kukua vizuri na kusababisha umeng’enyaji wa chakula ndani ya tumbo kuwa rahisi.

Lakini pia Dk Mandai anafafanua kuwa, kutokana na madini yaliyomo ndani ya zabibu huifanya divai kuwa dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminya kwa misuli ya kuta za matumbo (antispasmodic effect)

Mtaalam huyo anasema ni vizuri ukatumia kila siku japo punje za zabibu zisizopunguwa tano kwa ajili ya kulinda afya ya mfumo wa damu na nyama za moyo.

Hapa chini nimekuwekea picha za aina mbalimbali za zabibu zinazopatikana hapa duniani.
1 comment: