Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 31 January 2015

ZIFAHAMU FAIDA ZA MBUYU KWA AFYA YAKO
Mbuyu ni kati ya miti mikubwa na minene inayopatikana katika ukanda wa tropiki, Matunda yake yanaitwa mabuyu, gamba la tunda hilo huitwa kibuyu na ubuyu ni nyama ya tunda.
Mti huu umesheheni malighafi nyingi na nzuri katika afya ya binadamu, ambapo inaelezwa unga wa ubuyu huwa na vitamin na madini mengi, kwani unga huo una kiasi cha vitamin C nyingi kushinda ile inayopatikana kwenye chungwa.

Aidha, Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anabainisha kuwa mti huo wa mmbuyu husaidia kutibu homa, ambapo mgonjwa atapaswa kuchemsha magome yam mea huo.

Mtaalam huyo anaendelea kueleza kwamba mti huo unauwezo wa kutibu ugonjwa wa malaria, kifua kikuu  pamoja na pumu pale magome yake yanapotumika mara baada ya kuchemshwa.

Pamoja na hayo, Dk Mandai anafafanua kuwa kwa wale wenye shida ya kikohozi wanapaswa kuchanganya unga wa tunda lake pamoja na asali kisha mgonjwa atalamba au kutumia kwa kuchanganja na maji ya moto.

Mazao yatokanayo na mti wa Mbuyu. 

Hizo ni faida chache tu za mti wa mbuyu na mazao yake, lakini unashauriwa kufanya jitihada za kufika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam, ambapo kama unasumbuliwa na magonjwa sugu basi utapata suluhisho lako hapo.

No comments:

Post a Comment