Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 21 February 2015

ASALI PALE INAPOTUMIKA KUZUI TATIZO LA KUKOJOA KITANDANI KWA WATOTO
Katika hali ya kawaida mtoto anatarajiwa kuacha kukojoa anapofikisha miaka miwili hadi mitatu. 


Kuna sababu mbalimbali zinazofanya watoto wengine kuendelee kukojoa kitandani  hata baada ya umri huo.

Lakini moja ya sababu ya tatizo hili ni pale mtoto anapocheza sana wakati wa mchana na usiku  hivyo kulala bila kujitambua yaani akiwa amechoka sana.

Tatizo hili mara nyingi huwatesa sana wazazi wenye watoto wenye tatizo na hata watoto wenyewe pia hukosa raha na amni na hata kufikia hatua kuathirika kisaikolojia kutokana na shida hii.

Mtaalam wa tiba asili na Mkurugenzi wa kliniki ya Mandai Hebalist Clinic anasema kuwa tatizo hili huweza kuondoshwa kwa tiba mbalimbali ikiwemo matumizi ya asali pia.

Dkt Mandai, anabainisha kuwa kijiko kimoja cha mezani cha asali ndicho anapaswa kupewa mtoto na kulamba hadi amalize kabla ya kwenda kulala.

Tiba hii inapaswa kuzingatia kutumiwa kwa muda wa mwezi mmoja.

Vitu vinginea ambavyo huweza kusaidia tatizo hili kwa mtoto ni ndevu za mahindi, vitunguu maji, na ufuta mweusi.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment