Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 17 February 2015

BAADA YA EBOLA KUPUNGUA SASA SHULE ZAFUNGULIWA NCHINI LIBERIA
Shule nchini Liberia zimeanza kutoa mafunzo baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kufuatia mlipuko wa ugomjwa wa Ebola.


Shule hizo zimefunguliwa tena nchini Liberia, baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola. Hatua hiyo inakuja baada ya kupungua kwa visa vipya vya maambukizi ya ugonjwa huo.

Lakini wakati watoto wengi wanaelekea madarasani, hatua za kiafya zilizochukuiwa kudhibiti ugonjwa huo zimesababisha baadhi ya wanafunzi kutojumuika na wenzao kwa mafunzo.

Aidha, afisa mmoja wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Watoto UNICEF alisema kuwa, wanafunzi wengi wamerejea shuleni, lakini walimu katika shule kadhaa walishuhudiwa wakichukuwa hatua za tahadhari.

Walimu wakiwapokea wanafunzi baada ya kufungwa shule kwa muda mrefu
Pia wanafunzi walilazimishwa kunawa mikono yao kabla ya kuingia darasani huku viwango vya joto vikichukuliwa kutoka kwa kila mwanafunzi na waalimu nao waliwaeleza wanafunzi jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo wa ebola.
Wanafunzi wakifanyiwa kipimo kabla ya kuingia darasani
Shirika la UNICEF limekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii kuhusiana na mbinu za kuzuia ugonjwa huo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu tisa katika mataifa ya Guinea, Sierra Leone na Liberia.

No comments:

Post a Comment