Friday, 13 February 2015

BIZARI INAUWEZO WA KUTIBU SURUAKwa kawaida ugonjwa wa surua huwapata zaidi watoto wadogo chini ya miaka saba, na kwa watoto wenye umri wa zaidi ya miaka saba hutokea mara chache sana. 

 
Surua inaambukiza kwa njia ya virusi na ni ugonjwa unaoambukiza haraka sana ambao huambatana na dalili zake za mwanzo kama kuonekana majimaji ndaniya macho, kikohozi kikavu sana

Lakini baada ya siku kama nne hivi viupele vingi vidogo vidogo hutokeza sehemu za usoni na shingoni na baadaye kusambaa katika mwili mzima.

Katika hali mbaya zaidi ya ugonjwa wa surua huweza kuambatana na kuharisha, vidonda mdomoni, vidonda kooni, majipu ndani ya sikio.
 
Mtoto mwenye surua
Hata hivyo, mara nyingi mtoto anayepata lishe inayostahili huwa ni vigumu kuugua surua.

Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema moja ya tiba ambayo huweza kusaidia kukabiliana na surua ni utumiaji wa bizari.

Dk Mandai anafafanua kuwa, chukuwa kijiko cha chai cha unga wa bizari kisha changanya na kijiko kimoja cha chai cha asali na kijiko kimoja cha juisi ya karela. Kisha mpe mgonjwa anywe na tiba hii ifanyike asubuhi na mchana ndani ya siku saba.

Mbali na tiba hiyo Dk Mandai anasema pia machungwa, limau yanapotumiwa vizuri kwa kuchanganywa na baadhi ya vitu huweza kuwa tiba nzuri pia ya surua.Fanya jitihada za kufika Mandai Herbalist Clinic na upata tiba asilia zitokanazo na mimea na matunda. Au piga simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.

No comments:

Post a Comment