Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 12 February 2015

BORESHA AFYA YA NYWELE ZAKO KWA KUTUMIA TUI LA NAZI
Wanawake wengi wamekuwa wakihangaika katika kuhakikisha kuwa wanatunza nywele zao dhidi ya matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na mba au kukatika kwa nywele jambo ambalo limekuwa likiwagharimu pesa pia.


Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema kuwa njia mojawapo ya kuboresha nywele zako ni kuziosha nywele kwa tui la nazi, ambapo anasema kuwa mara baada ya kuosha nywele zako vizuri, ukachukuwa tui la nazi lililochunjwa vizuri na uoshee nywele zako huku ukihakikisha tui hilo linafika hadi kwenye vishina vya nywele.

Mtaalam huyo anaendelea kubainisha kuwa tui hilo litakuwa ni tiba nzuri kwa ajili ya tatizo la mba na kuzifanya nywele zako kukua kwa haraka zaidi na kuzifanya zionekane zenye afya tele.

Mbali na mafuta hayo ya nazi, Dk Mandai anasema kuwa mbegu za ndimu na pilipili manga zikichanganywa pamoja na kupondwapondwa na kisha kuchanganywa na tangawizi, mchanganyiko huo husaidia sana kuotesha nywele endapo mhusika atapaka kila siku jioni.
Vitu vingine ambavyo vinaweza kurutubisha nywele zako ni pamoja na ndimu, ufuta na mafuta ya nazi.

Karibu Mandai Herbalist Clinic endapo unasumbuliwa na maradhi sugu na utapata ufumbuzi wa tatizo lako. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment