Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 9 February 2015

DALILI ZA MWANAUME KUWA NA TATIZO LA KUSHINDWA KUFIKA KILELENI
Wiki iliyopita kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii utakumbuka tulizungumzia juu ya tatizo la wanaume kushindwa kufika kileleni na tulianza kuangalia sababau za tatizo. Sasa leo ni vizuri tuendelee na nimalizie kukupatia sababu za tatizo hilo pamoja na dalili na namna ya matibabu yake.Karibu.


Sababu nyingine inayoweza kuchangia tatizo hili kwa wanaume ni endapo mwanaume utafanyiwa upasuaji, hususani wa tezi dume au hata kiungo chochote cha uzazi, huweza kupelekea tezi dume isifanye kazi kama inavyotakiwa na hatimaye kusababisha mwanaume kutofika kileleni.

Pia masuala ya unywaji pombe kupita kiasi huchangia tatizo hili, lakini pia na hata matumizi ya madawa ya kulevya ambayo kwa namna moja au nyingine huweza kusababisha mishipa ya fahamu kushindwa kufanya kazi vizuri na kusababisha mwanaume kushindwa kufika mshindo katika tendo.

Matumizi ya baadhi ya madawa nayo ni moja ya sababu inayoweza kuchangia tatizo hili, madawa hayo ni kama yale matatizo ya presha, kisukari nk. Ingawaje si mara zote huweza kuwa sababu ya tatizo hili. 

Mara nyingine tatizo hili huwakumba wanaume kutokana na kuishi wakiwa na hofu, wasi wasi na msongo wa mawazo, mambo hayo pia ni sababu kubwa ya kumfanya mwanaume kutofika kileleni. Wasi wasi huo huweza kuwa wa kuhofia kupata maradhi, kufumaniwa au kusababisha mimba.

Mbali na sababu hizo pia sababu nyingine ni kuhusu historia mbaya ya mapenzi, inawezekana aliwahi kutendwa vibaya katika mapenzi au kubakwa n.k, hivyo sababu kama hizo pia huchangia tatizo hili kwa wanaume.

Lakini uchovu wa mwili ni chanzo pia cha tatizo hili na kupelekea mwanaume kukosa msisimko wa kutosha na hivyo kusababisha utokaji wa manii ukawa wa shida na endapo zitatoka basi mwanaume anaweza kutopata taarifa.

Sasa tuangali dalili za tatizo hili la wanaume kushindwa kufika kileleni, ambapo miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na mwanaume kuchukua muda mrefu zaidi ya dakika arobaini kutoka kwa manii, lakini pia mwanaume anaweza kufika kileleni pale anapojichua (masturbation), lakini pale anaposhiriki na mpenzi wake anakuwa hawezi kufika mshindo. Pia mwanaume hukosa hisia wakati wa utokaji wa manii.

Tatizo hili matibabu yake hutegemeana na chanzo cha tatizo, hivyo mhusika anapohisi dalili ni vizuri akafika hospitali na kuwaona wataalam.

Tatizo hili lisipopatiwa ufumbuzi husababisha upungu wa nguvu za kiume, na kukosa hamu kabisa ya kushiriki tendo la ndoa, madhara mengine husababisha kuvunjika kwa ndoa, mwanaume kushindwa kusababisha ujauzito, pamoja na msongo wa mawazo ambao huweza kusababisha magonjwa mengine kama shinikizo la damu, vidonda vya tumbo nk.Hivyo ni vizuri ukaonana na watalaam, lakini pia unaweza kufika kituo chetu kiiitwacho Mandai Herbalist Clinic kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Karibu

No comments:

Post a Comment