Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 14 February 2015

DOLA MILIONI 14 ZA EBOLA HAZIJULIKANI ZILIPOSerikali ya Siera Leone imesema kuwa inazingatia sana ripoti maalum iliyobainisha kwamba, takribani dola milioni 14 zilizopaswa kutumika katika kupambana na ugonjwa wa ebola hazijulikani zilipo.


Hayo yamebainishwa na msemaji wa serikali ya nchi hiyo, Abdulai Bayraytay alipokuwa akiiambia BBC, ambapo amesema kuwa yeyote ambaye atapatikana kuhusika kwenye ufisadi huo basi atakabiliwa na mkono wa sheria.
Naye mhasibu mkuu nchini humo ameishtumu Wizara ya Afya na Idara inayohusika na ugonjwa wa ebola kwa kile alichokitaja kuwa ni ukiukaji wa sheria.

No comments:

Post a Comment