Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 18 February 2015

EBOLA:HATIMAYE WATU 40 WATAJWA KWA RUSHWA SIERRA LEONE
Baada ya hivi karibuni nchini Sierra Leone kuripoti kupotea kwa dola milioni 14 zilizopaswa kutumika katika kupambana na ugonjwa wa ebola, hatimaye Tume ya Kuzuia Rushwa nchini humo ACC imewaamuru watu 40 kufika katika ofisi zake.


Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya ripoti ya ukaguzi kutolewa ikituhumu kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu katika kusimamia fedha za nchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.

Aidha, Mkuu wa ACC, Joseph Kamara amesema kuwa watu hao 40 ni sehemu tu ya idadi kubwa ya watu wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa nchini Sierra Leone, huku akisema wameanzia chini kupanda juu katika uchunguzi wao. 

Pia, Kamara alisema kuwa kundi lifuatalo litaitwa na ofisi yake mara baada ya watuhumiwa wa sasa kuchunguzwa na kushitakiwa pale unapopatikana ushahidi wa kutosha.

Hata hivyo, amri hiyo imekuja baada ya chama tawala cha All People's Congress kutoa wito wa kuwazuiwa kusafiri nje kwa watu wote waliotajwa katika ripoti hiyo.

Mbali na hayo, ripoti hiyo imewasilishwa mbele ya bunge la nchi hiyo ili kujadiliwa na kwa upande mwingine mwandishi wa BBC kutoka mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, Umaru Fofana amesema ripoti inawajumuisha maafisa waandamizi kutoka wizara ya afya, wafanyabiashara na wanaharakati wa vyama vya kijamii ambao ripoti hiyo imedai kuwa walipokea fedha kwa ajili kutumia katika kampeni dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

Karibu utangaze nasi kwa gharama nafuu sana, tafadhali fanya maamuzi sasa ya kututafuta kwa namba za simu zifuatazo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com  na utaamini kuwa sisi gharama zetu ni nafuu.

No comments:

Post a Comment