Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 24 February 2015

ENDELEA KUZIFAHAMU SIFA NYINGINE ZA KABICHI KATIKA TIBA
Kabichi ni mboga ya majani ambayo inafaida nyingi katika miili yetu kiafya.


Miongoni mwa faida za kabichi ni kusaidia katika kupunguza unene, na sifa hiyo inatokana na kalori ndogo ilizonazo na ufumwele wingi. 

Mbali na faida hizo pia kula kabichi huweza kumsaidia mtu kuukinga mwili dhidi ya magonjwa hatari ikiwemo saratani.

Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee wa kupambana na ugonjwa huu  kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za mada za 'Antioxidant', 'Anti-inflammatory' na 'Glucosinolates,' ambazo zina uwezo wa kudhibiti  magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.

Hivyo kutokana na madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatia upatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuza ulaji wake. 

Kabichi pia ni mboga yenye kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin hasa vitamini K, B1, B2, vitamin A na C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha ufumwele au kamba lishe kwa maana ya fiber, ambapo vyote hivyo ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi. 

Pia kabichi inakinga dhidi ya ugonjwa wa saratani, hususani inapotumika juisi yake. Miongoni mwa faida za juisi hizo ni ni kusaidia usagaji mzuri wa chakula.

Sasa tupo tayari kuanza kupokea matangazo ya biashara yako yoyote na kukuwekea kwenye tovuti hii inayotembelewa na maelfu ya watu. Karibu sana gharama zetu ni nafuu sana piga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment