Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 18 February 2015

FAHAMU FAIDA ZA CHENZA NA PALE LINAPOTUMIKA KATIKA TIBA
Chenza ni moja ya tunda lenye ladha nzuri sana na lenye kupendwa na watu wengi wakiwemo watoto na watu wazima pia.


Tunda hili wengi wetu tumekuwa tukilitumia sana huenda kutokana na kupenda ladha yake tu, lakini hili ni moja ya tunda ambalo pia lina faida nyingi katika miili yetu.

Miongoni mwa faida za chenza ni pamoja na kusaidia kuongeza vitamin C mwilini kama ilivyo katika chungwa, pia husaidia kuongeza nguvu kwenye misuli na kuimarisha mifupa.

Tunda hili pia husaidia kuzuia uvujaji wa damu katika fizi, na huondoa maumivu ya viungo sambamba na kuwasaidia wale wenye udhaifu wa kuona.

Mbali na hayo, pia chenza huwasidia wale wenye tatizo la mawe ya figo na kibofu, viuvimbe chini ya tumbo na inatibu unene wa mirija ya damu.

Matumizi yake katika tiba ni wewe kuzingatia kula kila unapoweza kulipata tunda lake.


Unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic endapo unasumbuliwa na magonjwa yoyote na hakika utapata tiba nzuri na sahihi na kupona kabisa shida inayokusumbua. Kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Au piga simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com 


No comments:

Post a Comment