Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 18 February 2015

FAHAMU HAYA MACHACHE KUHUSU HOMA YA MANJANO NA TIBA YAKE ASILI
Homa ya manjano ni ugonjwa wa kuambukukiza ambao hushambulia zaidi ini na kwa kawaida ugonjwa huu huwa hauoneshi dalili zozote katika hatua za mwanzo.

Ugonjwa unapoendelea unaweza kusababisha makovu katika ini na baada ya miaka mingi ini linapata makovu (cirrhosis) kwa wagonjwa wengine vidonda hivyo huweza kuwasababishia ini kushindwa kufanya kazi.


Matibabu ya ugonjwa huu ni muhimu kuhakikisha ini linarudishiwa katikautendaji wa kazi zake vizuri, kwa kuacha vichocheo vyote vya athari za ini. Huku mapumziko ya siku 10 hadi 14 yakiwa ni ya muhimu sana wakati wa matibabu yanapoendelea.

Kama nilivyosema hapo awali kuwa, mara nyingi ugonjwa huu huwa hauoneshi dalili za moja kwa moja, lakini mgonjwa huweza kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, uchovu, maumivu ya viungo au misuli na kupungua kwa uzito wa mwili. 
Mbaazi inaelezwa kuwa inauwezo wa kutumika kama tiba ya ugonjwa huu. Hii ni pale inapo pondwa pondwa gramu 200 za majani yake kisha kuongezwa maji glasi tatu na uchanganye vizuri kwa muda wa dakika 10.
 
Baada ya hapo chuja ili kupata juisi yake, kisha apatiwe mgonjwa nusu glasi ya juisi hiyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku 10 hadi 14 na wakati matibabu hayo yakiendelea kila siku hakikisha unapata glasi mbili za maziwa mtindi yaliyochanganywa na vijiko viwili vya mezani vya asali.

Pamoja na hayo, tiba nyinginezo ni nyanya na pilipili manga, mchunga, miwa pamoja na majani ya kijani ya radishi.

No comments:

Post a Comment