Thursday, 5 February 2015

FAHAMU MADHARA YA KUTUMIA VIJITI VYA KUTOA UCHAFU KWENYE MENO
Watu wengi hutumia vijiti vya kuchokoa meno maarufu kama ‘toothpick’ ikiwa kama njia nyepesi zaidi ya kuondoa mabaki ya vyakula mbalimbali kwenye meno.


Ingawaje kuna baadhi ya watu ambao hutumia vijiti hivi hata kama wamekwishaondoa mabaki ya vyakula kwenye meno, huku wakiona kama ni fashion au raha kutembea huku wakikitafuna kijiti hicho.

Lakini ni wazi kuwa kunaathari nyingi za kutumia vijiti hivyo ambazo miongoni mwa hasara hizo ni pamoja na kusababisha fizi kutanuka hivyo kuwa hifadhi ya mabaki ya chakula ambayo yakioza huwa chanzo cha kuharibu meno, lakini pia huharibu nafasi ya kati ya jino na jino.

Aidha, mtu anayetumia toothpick mara kwa mara hupata vidonda mdomoni kutokana na mikwaruzo na mara nyingi, mtumiaji anaweza asihisi kama amepata jeraha, lakini baadaye ndio unanza kuhisi amepata vidonda na kumbe vimesababishwa na toothpick na vidonda hivyo huweza kukua hasa pale bakteria wanapoingia kupitia uchafu ule ule ulio katika meno.

Madhara mengine ni fizi kuvuja damu mara kwa mara kutokana na tabia ya kuchokoa kila baada ya kula, lakini pia mbali na madhara hayo utumiaji wa vijiti hivi ni hatari endapo ikatokea kwa bahati mbaya ukimeza na inapotokea hivyo, huweza kusababisha baadhi ya ogani mwilini kushindwa kufanya kazi au kuharibiwa kwa utumbo.

Pamoja na  hayo iinaeleza kuwa kutafuna vijiti vya kuchokoa meno, husababisha kubaki kwa vipande vidogo vidogo ambavyo huweza kumezwa kwa bahati mbaya na mhusika na iwapo vitaingia katika ogani yoyote mwilini huweza kusababisha maumizu makali au hata  kifo.

Pamoja na hayo, vijiti hivyo pia vinaweza kuwa moja ya chanzo cha magonjwa kwani wengi huwa tunavitumia baada ya kuvikuta hata katika mazingira tusiyoyafahamu hasa katika migahawa. Hivyo ni rahisi kupata maambukizi ya magonjwa kwa njia hiyo kutokana na kuwa na ncha kali ya vijiti hivyohuweza kusababisha jeraha kwenye fizi au mdomoni na iwapo kilikuwa katika mazingira machafu basi bakteria wataingia moja kwa moja.

Wataalam wanashauri kama unahitaji kutoa uchafu katika meno ni vizuri ukatumia uzi katika zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment