Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 23 February 2015

FAHAMU NAMNA BORA YA KUTUNZA MENO YA MTOTO WAKO
Matunzo ya meno ya meno ya watoto yanahitaji uangalizi mkubwa kama ilivyo kwa watu wazima.


Pale inapotokea kupuuzwa kwa uangalizi wa meno ya watoto basi kunaweza kujitokeza kwa madhara ya muda mrefu maishani.

Madaktari wa meno wanashauri kuwa, ni vyema meno ya watoto yakaanza kusafishwa tangu pale linapochomoza au kuota jino la awali kinywani na ikiwezekana hata kabla ya hapo.

Kuhusu hili la kusafisha meno ya watoto wataalam wamekuwa wakishauri wazazi kutumia kitambaa na maji safi kusafishia meno ya mtoto, huku akiwa ameketi katika hali ya utulivu.

Wazazi pia wanapaswa kuzingatia usafi wao wa kinywa pamoja na wa watoto wao. Kutokana na vijidudu vya maradhi ya meno kupatikana ndani ya mate na hivyo ni rahisi kuenezwa kutoka kwa mzazi hadi kwa moto wakati wa kubusiana au kupitia uchangiaji wa vyombo vya chakula.

Aidha, mzazi anapaswa kusimamia afya ya kinywa cha watoto hadi pale mtoto anapofikia umri wa kati ya miaka nane au tisa, hapo ndipo angalau mtoto huweza kujisimamia katika kuboresha usafi wa meno unaotakiwa.

Pia madaktari wa meno wanasema kuwa, meno ya mtoto hupaswa kuanza kusafishwa kwa mpangilio angalau mara mbili kwa siku, kila baada ya kifungua kinywa na kabla ya kulala, yaani usiku, bila ya kusahau ulimi. 


Endapo meno ya mbele ya mtoto wako yameota, unashauriwa kutumia mswaki mdogo wa watoto na unapomsafisha hakikisha kuwa kichwa cha mtoto kimejiegemeza kwenye mapaja yako, ili uweze kuona vyema ndani ya kinywa chake na kuyasafisha vizuri, huku mtoto akiwa katika hali ya utulivu.

Ni dhahiri kuwa kwa sasa kuna aina mbalimbali za dawa za kusafisha meno (tooth paste) hivyo wazazi wanaweza kuwa na wakati mgumu katika kuchagua dawa sahihi katika utunzaji wa meno ya watoto, lakini jambo la muhimu na msingi hapa ni kufahamu kiasi kinachotawa kutumika katika mswaki wa mtoto wako na si aina ya dawa.

Kiasi kidogo tu cha dawa ya meno ndicho hutakiwa kwa mtoto wako na si lundo la dawa, vile vile dawa ya meno haipaswi kumezwa. 

Usafi wa kinywa si kwamba humsaidia mtoto kuharibika na kuoza meno, bali humfanya mtoto kukuwa katika afya njema zaidi.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbal Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.   

No comments:

Post a Comment